MSHAMBULIAJI Cristiano Ronaldo ameziweka
kiporo Manchester United na Paris Saint-Germain baada ya kusema
hataongeza Mkataba Real Madrid baada ya 2015.
Real imegoma kumuuza Mreno huyo msimu huu wakati United na PSG zinabakiwa mstari wa mbele atakapotiwa sokoni.
Alex Ferguson alimuuza Ronaldo kwenda
Madrid mwaka 2009, lakini nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 ameeleza
mara kadhaa hivi karibuni kwamba hana furaha sana katika Jiji hilo na
Hispania.
Cristiano Ronaldo amesema hataongeza Mkataba baada ya 2015
Rais wa Madrid, Florentino Perez alisema
anatarajia kuona Ronaldo akitungikia daluga zake katika klabu hiyo,
lakini inaonekana atatafuta klabu nyingine miaka miwili ijayo.
Ikiwa Ronaldo atakuwa mkweli kwa kauli
zake, ataondoka bure, kitu ambacho Madrid hawatapenda baada ya kumsajili
kwa Pauni Milioni 80.
United sasa inaelekeza nguvu zake kwa
kiungo wa PSV Eindhoven mwenye thamani ya Pauni Milioni 25, Kevin
Strootman, anayechezea pia timu ya taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 21 ya Uholanzi.
Manchester City nayo inataka kumsajili Mreno mwenzake Ronaldo, Pepe anayechezea Real pia wiki ijayo.
Pepe anatakiwa na Manchester City
0 comments:
Post a Comment