Na Mwandishi wetu
MASHINDANO
ya Redds Miss Kanda ya Mashariki yatafanyika Juni 29 Nashera Hotel
mkoani Morogoro kwa kushirikisha jumla ya warembo 14.
Mkurugenzi
wa kampuni ya Nikalex Ltd, Alex Nikitas aliwataja warembo hao ambapo
wapo kambini hotel ya Starwing Hotel chini ya mkufunzi, Kudra Lupatu
kuwa ni Muzne Abduly (19), Ummy Mohamed (21), Sabra Islam (19) na Diana
Laizer ambao wote wanatoka Morogoro.
Warembo
ambao wanatoka Mtwara kwa mujibu wa Nikitas ni Ivony Stephen (22),
Purkeriah Ndovi (21), Zulfa Semboja (19) na wa Lindi ni Janeth Awet
(19), Zainab Shaaban (23) na Sophia Mganga (21). Wanaotoka mkoa wa
Pwani ni Elizabeth Perty (22), Suleiyah Abdi (22) na Easther Albert
(20).
Nikitas
alisema kuwa maandalizi ya mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Redds
Original, Dodoma Wine, CXC Africa, Nyumbani Park, Usambara Safari Lodge,
Michuzi Blog, Clouds Media Group, Chilakale Resorts, Nashera Hotel,
Starwing Lodge, Simple car Rental, Big Solution na Mikocheni Resort
Centre yamekwisha kamilika na warembo watatembelea sehemu mbali mbali
mkoa wa Morogoro na kufanya kazi za jamii.
“Tumejiandaa
vziuri na warembo kwa sasa wapo kambini wakijifua kwa ajili ya shindano
hilo, warembo watatu wataiwakilisha kanda hiyo katika mashindano ya
Redds Miss Tanzania ambayo yatafanyika mwezi Septemba,” alisema Nikitas.
Alisema
kuwa wamejipanga vilivyo kwa ajili ya mashindano hayo ambayo
yanatarajiwa kuwa na ushindani mkali kutoka kwa warembo wote.
0 comments:
Post a Comment