NA RAMADHANI ALI /HABARI MAELEZO ZANZIBAR
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Muhammed Shein
amesema ziara yake ya wiki moja nchini China itaisaida sana Zanzibar
katika kuimarisha uhusiano kati ya nchi hiyo na Zanzibar na
kuharakisha maendeleo ya wananchi.
Akizungumza
na waandishi wa habari baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Kimataifa
wa Abeid Amani Karume, Dk. Shein amesema katika ziara hiyo amefanya
mazungumza na viongozi wa juu wa China akiwemo Rais, Makamu wake na
Waziri Mkuu wa nchi hiyo ambayo yalilenga kuimarisha uchumi wa
Zanzibar katika sekta mbali mbali za maendeleo.
Amezitaja
sekta hizo kuwa ni pamoja na Afya, Kilimo, Huduma za Elimu na Biashara
pia waliangalia uhusiano katika maeneo mengine mapya ya uvuvi wa bahari
kuu na uwekezaji vitega uchumi.
Dk.
Shein amesema China na Zanzibar wamekubaliana kuimarisha sekta ya
Biashara ambapo Naibu Waziri wa Biashara wa China ameitaka Zanzibar
kuandaa rasimu ya mapendekezo ya miradi ambayo itashughulikiwa na nchi
yake.
Akizungumzia
Kilimo Rais Shein amesema wamekubaliana na China kuja kufanya utafiti
wa uvuvi wa bahari kuu, kusaidia utaalamu na kuwekeza miradi mikubwa
katika sekta hiyo.
“
Uvuvi unanafasi kubwa katika maendeleo ya Zanzibar lakini tunahitaji
uvuvi wa kisasa wenye tija, na kuanzisha miradi ya ufugaji samaki na
yote haya wenzetu wamekubali, ” amesema Dk.Shein.
Amesema
Zanzibar imepeleka wavuvi wadogo wadogo 59 wa vijiji vya Unguja na
Pemba kujifunza nchini China na waliporudi wamewaelimisha wavuvi wenzao
na tayari mafanikio yameanza kuonekana.
Ameongeza
kuwa katika mazungumzo yake na viongozi wan chi hiyo amewataka
kuimarisha sekta ya Utalii kwa kuitangaza Zanzibar na kuwashajiisha
wananchi wa nchi hiyo kufanya ziara za kitalii nchini.
Rais
wa Zanzibar amesema katika kufanikisha ziara hiyo Ujumbe mkubwa kutoka
China utawasili Zanzibar muda mfupi ujao kuangalia maeneo ya uwekezaji
na ametaka wahusika kujiandaa.
“Lazima
tubadilike na tujiandae wenzetu hawako katika mchezo katika uwajibikaji
na ndio maana nchi yao inapiga hatua kubwa ya maendeleo, ” amesema Rais
wa Zanzibar.
Akizungumzia
ujenzi wa Uwanja wa ndege wa Zanzibar uliokuwa ukifanywa na Kampuni ya
Ujenzi kutoka China na ambao umekwama, Dk. Shein amesema yapo mategemeo
makubwa ya kuanza tena muda mfupi ujao baada ya mshauri muelekezi
alieletwa na Zanzibar kutoka Ufaransa kukamilisha kazi yake.
Dk.
Shein na ujumbe wake waliondoka Zanzibar tarehe 27 mwezi uliopita na
katika ziara hiyo aliungana na viongozi wengine kutoka Sirilanka, Papua
New Guinea, Singapore na Malaysia katika mkutano mkubwa wa Kimataifa
wa Biashara uliofanyika nchini humo.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.
0 comments:
Post a Comment