Saturday, June 15, 2013

Kevin-Prince Boateng © Gallo Images

Rais wa chama cha soka nchini Ghana Kwesi Nyantakyi amethibitisha kuwa mchezaji wao Kevin Prince Boateng ameomba kurejea timu ya taifa ya nchi hiyo maarufu kama Black Stars.
Mchezaji huyo wa AC Milan ya Italia alitangaza kujiweka kando na timu ya taifa ya Ghana mara baada ya kumalizika kwa fainali za kombe la dunia nchini Afrika Kusini mwaka 2010.
Rais wa soka wa Ghana amesema kurejea kwa mchezaji huyo kwa kikosi cha taifa itakuwa faraja kubwa kwani amesema yuko fiti kwa ajili ya mechi mbalimbali zinazoikabili timu hiyo.
Watoto wa Pele nao warejea kikosini Black Stars
Andre na Jordan Ayew kwa pamoja wamekubali kurejea nyumbani baada ya kufanya mashauriano na rais wa Ghana John Mahama mjini Accra.
Ndugu hao wawili walitangaza kuwa hawataichezea tena timu ya taifa ya Ghana mwezi Februari, baada ya kutofautiana na wasimamizi wa timu hiyo ya taifa ya Black Stars.
Ripoti zinasema wachezaji hao wawili wa klabu ya Marseille ya Ufaransa walifanya mazungumzo na rais Mahama wakati alipokuwa ziarani nchini Ufaransa.
Na katika mkutano wao wa pili, hii leo wachezaji hao waliafikiana kurejea tena nyumbani ili kuichezea Black Stars.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video