Na Baraka Mpenja kwa masaawa wa Sportsmail.com
Mshambuliaji
hatari wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Ujeruman, Lukas Podolski
ameonekana kufurahia maisha ya jijini London katika klabu yake ya
washika bunduki, Arsenal, chini ya kocha mfaransa Arsene Wenger baada ya
kutumia akaunti yake ya Twita kuonesha picha zake akiwa katika dimba la
Emirates.
Mjerumani
huyo ameonekana kufurahia maisha The Gunner licha ya kuhusishwa na
uhamisho wa kwenda nyumbani kwao katika klabu ya Borrusia Dortmund.
Podolski
mwenye umri wa miaka 27, jana usiku akiwa na kikosi cha timu ya taifa,
wamepigwa mabao 4-3 na watoto wa Barack Hussein Onyango Obam, timu ya
taifa ya Marekani, lakini baada ya hapo alitumia muda wake mwingi kuweka
picha katika akaunti yake ya Twitaa akidhihirisha kuwa ana furaha kubwa
kukaa Emirates.
Akiwa
katika Rada: Dortmund wanammezea mate vibaya mno na kila kukicha
wanaitaka saini yake, si mwingine, ni kijana wa Arsenal, Lukas Podolski
ili kuziba pengo la Mario Gotze aliyetimkia kwa wekundu wa kusini mwa
Ujerumani, FC Bayern Munich
Si mchezo, patashika nguo kuchanika: Lukas Podolski na Ujerumani yake walitandikwa misumari 4-3 na watoto wa Obama
0 comments:
Post a Comment