Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akiagana na Balozi Mdogo wa China anayefanyia kazi zake Zanzibar Bibi Chen Qiman, katika uwanja wa Ndege wa Mji huo Nchini china,akirejea Zanzibar baada ya kumalizika ziara ya mualiko wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China jana. [Picha na Ramadhan Othman Xiamen China,]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,wakiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Mambo ya Nje ya Serikali ya Jimbo la Xiamen Hong Chengzong,katika uwanja wa Ndege wa Mji huo Nchini china,akirejea Zanzibar baada ya kumalizika ziara yake nchini humo jana. [Picha na Ramadhan Othman Xiamen China,]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Mkuu wa Kamapuni ya ufugaji wa Mazao ya Baharini aina ya Chaza Zheing Shubin,katika wilaya Xiang’an jimbo la Xiamen,alipowasili katika kampuni hiyo akiwa katika mualiko wa Serikali ya Jamahuri ya Watu wa China,[Picha na Ramadhan Othman,xiamen China,]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kulia akiwa na ujumbe wake wakiangalia Mazao ya Baharini Aina ya Chaza,mazao hayo yakufuga yanaendelezwa na kampuni ya Peiyang Ablone,katika wilaya ya Xiang’an iliyo katika mji wa Xiamen nchini China,Rais na ujumbe wakiwa katika ziara ya mualiko wa Serikali ya Watu wa jamhuri hiyo.[Picha na Ramadhan Othman Xiamen China,] Mabwawa yaliyotengenezwa katika mpangilio maalum ya kufugia Mazao ya Baharini aina ya Chaza katika kampuni kampuni ya Peiyang Ablone,katika wilaya ya Xiang’an iliyo katika mji wa Xiamen nchini China, [Picha na Ramadhan Othman Xiamen China,
0 comments:
Post a Comment