Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Kocha
mpya wa Manchester City, Manuel Pellegrini anatarajia kumpa mkataba
mwingine mchezaji nyota wa klabu hiyo, Mfaransa Samir Nasri.
Nasri amekaa City kwa misimu miwili tangua ajiunge na miamba hiyo akitoka kwa washika bunduki wa jiji la London Arsenal.
Kulikuwa
na taarifa zilizoenea kuwa klabu ya Man City anataka kumuuza Nasri ili
kupata fedha za kuwasainisha wachezaji wengine katika safu ya
ushambuliaji, lakini kocha Pellegrini amesema nyota huyo ana nafasi na
mchango kwa timu yake, hivyo anataka kumpa mkataba katika dirisha la
majira ya joto ya usajili barani Ulaya.
Bado
anahitajika: Samir Nasri (kulia) alikuwa na mahusiano mazuri sana na
kocha aliyetimuliwa kazi, Roberto Mancini na sasa bado anaonekana
kupendwa na kocha mpya, Manuel Pellegrini baada ya kutangaza kumpa
nafasi nyingine Etihad
Derby
ya Manchester: Nasri akipambana na Danny Welbeck katika mechi ya ligi
kuu soka nchini England ambapo City walishinda 2-1 mwezi wa tatu mwaka
huu
Inafahamika
kuwa kocha Pellegrini aliyejiunga rasmi na Man City mwishoni mwa wiki
iliyopita amemuambia mkurugenzi wa klabu hiyo, Txiki Begiristain kwamba
anaiona nafasi ya Nasri siku za usoni kama atapenda kubaki.
Tayari City wameshamsainisha Mhipania Jesus Navas na sasa wanapambana na Real Madrid kumuwinda nyota wa Malaga, Isco.
Bosi: kocha mpya wa Manchester City Manuel Pellegrini akiwa katika mkutano na waandishi wa habari
0 comments:
Post a Comment