Wednesday, June 12, 2013


Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Kocha mtarajiwa wa klabu ya Manchester City Manuel Pellegrini amekutana na mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo Txiki Begiristain pamoja na mkurugenzi mkuu Ferran Soriano ili kuweka sawa baadhi ya mambo kabla ya kutangazwa rasmi kurithi mikoba ya kocha aliyetimuliwa klabuni hapo Roberto Mancini.
City wanatarajiwa leo hii au kesho kumtangaza Pellegrini  kuwa bosi mpya wa miamba hiyo ya soka nchini England baada ya kukubaliana ana kocha huyo wa zamani wa klabu za Malaga na Villarreal za nchini Hispania.
Usiku wa jana, City walithibitisha kumsainisha mkataba winga machachari wa Sevulla, Jesus Navas kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 14.9
Baada ya kusaini City, Navas mwenye umri wa miaka 27 alisema ” Manchester City ni timu inayonifurahisha sana, nafikiri ni wakati wangu muafaka kuifanyia makubwa”.
Kocha mpya wa City, Pellegrini anatarajiwa kufanya mazungumzo na wachezaji Carlos Tevez, Gareth Barry na Joleon Lescott ili kuwasajili kwa ajili ya msimu ujao.
City watasafiri kwenda Afrika kusini, Hong Kong na Helsinki kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu nchini England pamoja na michuano mingine barani Ulaya.
Incoming: Manuel Pellegrini will join Manchester City in the coming days  
Bosi Mpya: Manuel Pellegrini anatarajiwa kujiunga na City siku chache zijazo
New boys: Jesus Navas (above) and Fernandinho (below) have already joined City this summer  
Mashine mpya: Jesus Navas (juu) na  Fernandinho (chini) tayari wameshajiunga na klabu ya Manchester City kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu nchini England

New boys: Jesus Navas (above) and Fernandinho (below) have already joined City this summer

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video