Sunday, June 23, 2013

arusha-bomb 
Na Gladness Mushi ,Arusha
SERIKALI imetangaza kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote walioshiriki katika tukio la bomu Arusha,kwa kununuliwa kifedha pia itahakikisha  kuwafuatialia hatua kwa hatua waliosababisha vifo vya
watu wasio na hatia.
 Naibu waziri wa mali asili na utalii Lazaro Nyalandu aliyasema hayo jana jijini Arusha wakati akizungumza na waandishi wa habari na kutoa msimamo wa wizara hiyo,kuwa pamoja na kutambua mchango wa vyombo vya
habari tangu tukio hilo itokee juni 15,mwaka huu wale wote walioshiriki watatiwa mbaroni bila huruma.
Nyalandu amesema serikali itahakikisha walioshiriki  tukio la bomu Arusha kwa  kununuliwa kwa fedha miundo mbinu mbalimbali iliyotumika watatafutwa na kuchukuliwa hatua za kisheria na kutokomeza kabisa
matukio ya kigaidi yanayotkea nchini.
Alisema taswira ya hali ya utalii Nchini kwa hivi sasa imeyumbishwa na matukio mawili jambo ambalo linawafanya watalii pamoja na wafanya biashara kushindwa kufanya shughuli zao kama kawaida.
“sote tunajua kuwa tukio la mei 5 katika kanisa la mt Joseph Mfanya kazi Olasiti ikiwa simepita siku chache hili nalo limekwamisha hali ya watalii kuingia nchini kupungua na wafanya biashara kushindwa kuendelea na shughuli zake kama ilivyokuwa imezoeleka”alisema Nyalandu.
Pamoja na hayo alisema endapo  hali ya utulivu hapa nchini haitaendelea wafanya biashara hawataweza kufanya kazi zao kwa uhuru,lakini endepo kutakuwepo na hali ya amani watalii watakuja katika mji wa Arusha kwa ailimia kubwa kama ilivyozoeleka na kuelekea katika kutebelea hifadhi za wanyama zilizopo chini ya Tanapa.
Alisema Tanzania kwa mara ya kwanza imefanikiwa kupokea watalii milioni moja kwa kipindi cha mwaka jana,Kenya wakiwa wanaongoza kwa milioni mbili hadi tatu.
Kuhusu hofu ya watalii kushindwa kuingia nchini kutokana na matukio ya kigaidi yanayotokea siku hadi siku,naibu waziri amesema serikali inajitahidi kufanya njia za kila namna kuona kuwa hali hiyo haiwezi kuathiri wageni wanaoingia nchini.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video