Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Nyota
wa Brazil Neymar Da Silva ametambulishwa leo katika klabu ya Barcelona
na kuungana na nyota wa miamba hiyo ya Dunia Andrew Lionel JorgE Messi
ambapo watacheza katika safu hatari ya ushambuliaji.
Nyota
huyo mwenye kipaji cha hali ya juu amesaini mkataba wa miaka mitano
kuitumiki klabu yake mpya baada ya kufanya kazi iliyotukuka katika timu
ya Santos ya kwao Brazil.
Neymar
alisafiri jana usiku baada ya kumalizika kwa mechi ya kirafiki ya timu
yake ya taifa ya Brazil dhidi ya England iliyomalizika kwa sare ya
kufungana mabao 2-2 na leo hii imefuzu vipimo katika klabu ya Barca na
kutambulishwa mbele ya umati mkubwa wa mashabiki wa klabu hiyo katika
dimba la Camp Nou.
Katika
mahojiano na waandishi wa habari baada ya kutambuliwshwa rasmi, Neymar
alisema “Nimekuja hapa kumsaidia na kumsaidia Messi ili aendelee kuwa
mchezaji bora wa dunia”.
Neymar
alisisitiza kuwa amefurahi sana kuwa mchezaji wa Barcelona kwani
ilikuwa ndoto yake, hivyo ataifanyia makubwa zaidi na kuifanya endelee
kuwa klabu bora zaidi duniani.
Kazi
imebaki kwa kocha Tito Vilanova kufanya maamuzi jinsi atakavyowachezesha
nyota hao wawili, lakini kiungo fundi Andres Iniesta ana uwezo wa
kuwalisha wote wawili mipira ya maana endapo watacheza pamoja.
Amefika kwa mafundi wenzake: Neymar ametambulishwa rasmi leo Camp Nou na kujiunga na nyota wa dunia Lionel Messi
Karibu Camp Nou: Mbrazil Neymar amesaini mkataba wa miaka mitano kuichezea Barca ya Messi
Nyota
huyo amefuzu vipimo vya afya na anatarajiwa kuanza kuitumika klabu ya
Kalalunya juni 28 mwaka huu, na leo hii amepimwa mbele ya rais wa Barca,
Sandro Rosell, Makamu wake, Josep Maria Bartomeu na mkurugenzi wa
michezo, Andoni Zubizarreta.
Maufundi ya kufa mtu: Neymar alionesha kipaji cha hali ya juu leo Camp Nou, alichezea gozi kama kazaliwa nalo
Mpaka sasa ada ya uhamisho haijawekwa wazi
Daaah! nyota huyu na mwenzake: Neymar anajiunga na Lionel Messi kuongoza safu hatari ya ushambukiaji ya Baraca
Fulu shangwe: Rais wa Barcelona, Sandro Rosell amemkaribisha Neymar, Nou Camp
Nyomi
kubwa mnooo!: Neymar akiwapungia mkono mashabiki wa Barcelona
waliofurika Camp Nou na kwa mara ya kwanza ametembea katika dimba hilo
Madogo wanaoshabikiwa Barca: Neymar akiwa hai mashabiki watoto wa Barca katika dimba la Camp Nou
Vipimo vya afya: Neymar amefuzu zoezi hilo.
0 comments:
Post a Comment