MWENYEKITI
wa Umoja wa vijana wa chama cha mapinduziTaifa (UVCCM), Sadifa Juma
Hamisi, amepinga vikali kuwepo kwa mfumo wa serikaliv tatu kama inavyopendeka rasimu ya katiba.
Sadifa
ameyasema hayo wakati akizungumza na wanachama wasomi wa UVCCM kutoka
katika vyuo vikuu mkoani kilimanjaro katika hafla ya kuwaaga wasomi hao
na ambapo pia ametunuku vyeti vya uanachama kwa wanafunzi 312 pamoja na kuwakabidhi kadi za uanachama wanachama wapya.
Mwenyekiti wa UVCCM Kilimanjaro akiongoza maandamano kuelekea katika ukumbi wa CCM mkoa ambapo ndipo ilikofanyikia mkutano mkubwa wa UVCCM jana |
Mwenyekiti
huyo ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Donge (CCM) zanzibar, amesema
uwepo mfumo wa serikali tatu ni mzigo mkubwa kwani kutokana na uduni wa
uchumi wan chi yetu itakuwa vigumu kuendesha serikali tatu kwa maana ya
serikali ya Zanzibar, serikali ya Tanzania bara na ule wa muungano.
Viongozi waandamizi wa CCM mkoani Kilimanajro katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa |
“Jamani
tusidanganyane, kuendesha serikali tatu ni mzigo, kwa uduni wa uchumi
wetu sidhani kama itakuwa rahisi kuendesha serikali tatu, kama kutakuwa
na serikali tatu kuna hatari ya kuvunjika kwa muungano wetu huu maana
uwezo kuchangia hatuna, tutajiingiza kwenye matatizo makubwa, vijana
tuwe makini na tutumie taaluma zetu kuhimiza umuhimu wa kuwepo kwa
muungano huu wa sasa,”
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Juma Hamisi Akipokea Maandamano ya Wanafunzi wa Vyuo vikuu Kilimanjaro ambao ni makada wa UVCCM mkoani Kilimanjaro |
Aidha Sadifa amewahimiza vijana kuwa mfano mzuri kwa jamii
huku akiwahimiza kuwa waadilifu, wazalendo, kujiamini na kuwa na
nidhamu hali ambayo itasaidia kuwepo kwa amani na usalama wa nchi.
Amesema bila amani na muungano wa wananchi maendeleo hayawezi
kupatikana katika nchi ambpo aliwataka vijana kuwa mtari wa mbele
kuwaelimisha wananchi wa kawaida juu ya umuhimu wa kuenzi, kudumisha na
kuimarisha muungano wa zanzibar na Tanganyika kama njia pekee ya
kuhakikisha nchi inakuwa na amani siku zote.
Katibu wa UVCCM manispaa ya Moshi, Bwana Makwaiya akisakata Rumba muda mfupi baada ya maandamano kuwasili katika makao makuu ya CCM mkoa wa kilimanjaro |
“Vijana
tuna wajibu kubwa wa kuwaenzi waliotuletea muungano wetu wa sasa,
taaluma zetu ziwe dira ya jamii katika kuenzi, kudumisha na kuimarisha
muungano wetu kwani ndio njia pekee ya kusaidia kudumisha amani na
usalama wan chi yetu, tuepuke kujiingiza katika mkumbo wa wale wanaodai
nchi haitatawalika,” amesema
Hata
hivyo Sadifa amewataka vijana kutodanganyika na vyama vinavyoeneza chuki
na maandamano yasiyokuwa na msingi wowote huku akifafanua kuwa kisheria
kuandamana na haki ya msingi lakini ifuate sheria na yassingilie haki za wengine.
Sadifa akikabidhi cheti cha unachama kwa mwanafunzi wa chuo kikuu muccobs jana, jumla ya wanavyuo 312 walipata vyeti vya uanachama wa UVCCM |
“Chama
pekee katika nchi hii ni CCM, kuna vyama vingine vimeanzishwa ambavyo
mimi binafsi naviita ‘Saccos’, hauwezi ukajikopesha fedha kienyejienyeji
kama alivyofanya Dk. Slaa! Vijana tuwe makini na saccos hizi ambazo
ajenda zao ni kukopeshana na vurugu tu,” amesema Sadifa
Kwa upande wake mwenyekiti wa shirikisho la wanafunzi wa
vyuo vikuu wanachama wa CCM kilimanjaro, Wakati Mtulya akizungumzia
changamoto wanazokumbana nazo, alisema kumekuwa na urasimu ndani ya bodi
ya mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, ambapo mikopo imekuwa ikitolewa
kwa watu wasiostahili huku walengwa wakiendelea kutaabika.
Mwenyekiti wa shirikisho la Vyuo Vikuu mkoani Kilimanjaro, Wakati Mtulya |
Amesema
kuwa kumekuwa na mchezo ndani ya bodi hiyo, ambapo mikopo imekuwa
ikitolewa kwa watoto wa matajiri huku wastahili ‘watoto wa wakulima’
wakibaki kuzungushwa na kuwekewa masharti magumu ya kupata mikopo hiyo
jambo ambalo limekuwa likichangia kuwepo kwa vitendo vibaya miongoni mwa
wanafunzi hao.
Sadifa (aliyevaa suti) akiongoza vijana kucheza kwaito katika ukumbi wa CCM mkoa wa Kilimanjaro |
“Mikopo
ni yetu, sio ruzuku, lazima tukopeshwe kwa wakati kwani lazima
tutairudisha lakini jambo la kusikitisha, bodi hii imekuwa ikitoa mikopo
kwa watoto wa masaki, huku sisi watoto wea mkulima tukiendelea
kuzungushwa na kuwekewa masharti magumu ili kupata mikopo hiyo, hili ni
tatizo,” amesema Mtulya (habari na TAIFA LETU.com).
0 comments:
Post a Comment