Na Baraka Mpenja
Mlinzi
wa kushoto wa klabu ya Yanga ya Dar es salaam, Stephano Mwasyika
amekiri kumalizika kwa mkataba na mabingwa hao wa ligi kuu msimu
uliopita na kombe la Kagame , na kukiri kutokusaini mkataba mpya wa
kuwatumikia wanajangwani hao msimu ujao.
Mwasyika ameimabia MATUKIO DUNIANI
kuwa anamshukuru mungu kumaliza mkata na Yanga kwani ameishi kigumu
sana hasa msimu uliopita kutokana na kutoelewana na baadhi ya viongozi
wa klabu hiyo.
“Kwasasa
wanajangwani nimemalizana nao, sifikirii hata kidogo kuongeza mkataba,
mpira ni kazi yangu, lakini kwa Yanga mimi basi, acha niangalie mambo
mengine”. Alisema Mwasyika.
Akiongelea
maisha yake ya baadaye, Mwasyika amesema kuna timu kadhaa za hapa
Tanzania ambazo anafanya nazo mazungumzo, lakini kwa sasa hayuko tayari
kutaja timu hizo.
“Msimu
ujao nitacheza ligi ya hapa nyumbani, kama watatokea mawakala wa
kunitafutia timu nje ya nchi basi nitaenda, lakini bado nitakuwepo msimu
ujao. Timu mpya ambayo nitaichezea nitataja hapo baadaye”. Alisema
Mwasyika.
Mwasyika
alisema kuwa wachezaji wengi wanatamani kucheza Yanga na Simba ambazo
zina presha kubwa ya mashabiki, lakini yeye ameona hali halisi ya klabu
hizo, hivyo anatamani kutoka kwenda timu nyingine ili akacheze soka la
uhakika.
“Mara
nyingi timu kubwa zina fitina sana, kwa upande wangu siogopi kitu, hata
ikitokea penati naenda kupiga kama kawaida, lakini kwa ukweli watu
wengi wanaogopa sana kutokana na majungu ya watu”.
Kwa
wanaofuatilia mechi za Simba na Yanga, endapo timu itapata penati,
wachezaji wengi wanakimbilia kunya maji, lakini ukweli ni kwamba
wanafanya vile kukwepa lawama za mashabiki na viongozi.
“Watu
wanazuga tu, hakuna cha kunywa maji, ni uoga wa kupiaga penati, lakini
mimi katika maisha yangu siogopi, huwa napiga tu na sijawahi kukosa
penati”. Alijisifu Mwasyika.
Akizungumzia
msimu uliopita wa ligi kuu Tanzania bara, Mwasyika alisema ushindani
ulikuwa mkubwa ambapo amezitaja klabu za Kagera Sugar, Coastal Union,
Ruvu Shooting, kuonesha kandanda safi zaidi.
“Kuna
timu nyingi sana zinazofanya vizuri kwa sasa, lakini Coastal na Ruvu
zilicheza vizuri sana, nao Tanzania Prisons walijituma sana licha ya
kuathiriwa na ajali, pia Kagera walicheza vizuri sana”. Alisema
Mwasyika.
0 comments:
Post a Comment