Tuesday, June 11, 2013

Mrisho Khalfan Ngasa “Anko” akimunyoosha beki wa Ivory Coast katika moja ya mechi za nyuma

Na Baraka Mpenja 
Kufuatia timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa stars kupoteza mchezo muhimu ugenini dhidi ya Morroco kwa kufungwa mabao 2-1 katika mechi ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia mwakani nchini Brazil, wadau wameendelea kutoka maoni yao kwa mitazamo tofauti.
Miongoni mwa wadau ambao wamezungumza na MATUKIO DUNIANI ni katibu wa zamani wa shirikisho la soka Tanzania TFF aliyekaa madarakani kwa miaka minne, Fredrick Mwakalebela sanjari na kocha msaidizi wa maafande wa jeshi la kujenga taifa, klabu ya JKT Oljoro ya jijini Arusha, Riziki Shawa.
Mwakalebele kwa upande wake,  amesema kuwa Taifa Stars bado ina nafasi ya kufanya vizuri katika michezo yake iliyosalia katika  harakati hizo za kuwania kombe la dunia.
“Tunajua kuwa Stars ilipoteza mchezo dhidi ya Morroco, binafsi naiamini timu yetu, ilicheza vizuri sana, magoli waliyofungwa kufuatia uzembe na mabeki. Baada ya Agrey Moriss kuoneshwa kadi nyekundu, safu ya ulinzi ya stars iliyumba sana na ndio maana wakapoteza, lakini timu ni nzuri na itafanya vizuri”. Alisema Mwakalebela.
Katibu huyo wa zamani wa TFF aliongeza kuwa licha ya Stars kukabiliwa na mchezo wa nyumbani dhidi ya Tembo wa Pwani ya magharibi ya Afrika, timu ya taifa ya Ivory Coast yenye nyota wengi wanaokipiga medani ya kimataifa, bado vijana wanaweza kufanya maajabu na kuwaduza wakali hao wa Afrika.
“Ivory Coast ina wachezaji wengi wenye uzoefu mkubwa, pia wanacheza ligi kubwa barani ulaya, lakini wanafungika tu, mbona tuliwafunga wenzao wa Cameroon hapa nyumbani, mimi sina wasiwasi na kikosi cha Stars”. Alisema Mwakalebela.
Pia Mwakalebela amewaasa Watanzania kuiunga mkono timu yao katika mashindano haya muhimu, kwa kuanza,  wajitokeze kwa wingi kuishangilia Stars katika mchezo wa nyumbani dhidi ya Ivory Coast, mchezo utakaopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Kwa upande wa Riziki Shawa, amesema nafasi ya Stars ni finyu sana na wanatakiwa kujipanga kwa michuano mengine, lakini safari ya kwenda Brazil imeishia mikononi mwa Tembo wa Afrika.
“Unajua wakati wa kupeana moyo umepita na wakati, lazima ukweli ubaki pale pale, Stars kusonga mbele ni kazi ngumu sana, najua mpira unadunda, ila wenzetu wamekamilika sana na wanajua wanachokifanya”. Alisisitiza Mwakalebela.
Shawa alisisitiza kuwa miamba hiyo ya soka barani Afrika haiwezi kukubali kupoteza nafasi kirahisi, hivyo watacheza kwa kujituma na kutumia uzoefu wao mkubwa walionao katika soka la kimataifa.
“Baada ya kushinda mabao matatu 3-0 dhidi ya Gambia ambao walifungwa na Stars hapa nyumbani mabao 2-1, Ivory Coast wamepata nguvu zaidi, kwa uhakika wanapiga hesabu kali za kukutana na sisi, tusipoangalia tunaweza kulia hapa nyumbani”. Alisema Shawa.
Wakati wadau hao wakitoa maoni yao, kocha mkuu wa Taifa stars, Kim Paulsen amesema anakiamini kikosi chake mbali na kufungwa kigumu na Morroco nchini mwao.
Kim alisema amesahau kilichowakuta Morocco,  ila anapigia hesabu mchezo dhidi ya Tembo wa Afrika pamoja na “The Scorpion”  Nge, timu ya Taifa ya Gambia ugenini.
Msimamo wa kundi C; Ivory Coast wana pointi 10 katika nafasi ya kwanza, nafasi ya pili Taifa stars wapo na pointi 6, Morocco wapo nafasi ya tatu na pointi 5, huku Gambia wakiburuza mkia kwa kujikusanyia pointi moja tu kibindoni.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video