Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Mabingwa
wa ligi kuu soka nchini England, mashetani wekundu, Manchester United,
wamepata matumaini mapya wa kuwana nyota wawili, Cesc Febregas na Robert
Lewandowski baada ya wachezaji hao kukiri kuwa wanavutiwa na ligi kuu
ya England.
Meneja
mpya wa United, David Moyes anapenda kuwasajili wachezaji hao wawili
kutoka FC Barcelona na Borussia Dortmund kabla ya kikosi chake kuondoka
kwenda ziarani barani Asia na Australia katikati ya mwezi ujao.
Wachezaji
hao wenye kiwango cha juu, kwa nyakati tofauti wamekiri kuwa wanapenda
kucheza ligi ya England yenye ushindani mkubwa, hivyo United
wamefurahishwa na kauli za wachezaji hao na kujiongezea matumaini ya
kuwanasa katika dirisha la usajili la majira ya joto barani ulaya.
Fabregas
mwenye umri wa miaka ya 26 kwa sasa hajaonesha nia ya kurejea Arsenal
alipocheza kwa miaka 8 kabla ya kurejea FC Barca, hivyo United
wamejijengea imani kuwa nyota huyo atachagua Old Traford msimu ujao wa
ligi barani ulaya.
Kwa
upande wa Lewandowski, anataka kucheza nchini England baada ya dili la
kuhamia kwa mabingwa wapya wa ligi ya mabingwa barani Ulaya, Fc Bayern
Muinch kugonga mwamba kwa madai ya Dortmund kukataa kupeleka muuaji
mwingine kwa wapinzani wao wakubwa katika ligi ya Bundesliga.
Hivi
karibuni Dortmund imemuuza mshambuliaji wao hatari Mario Gotze kwa
Bayern Munch, hivyo kuwapa tena Lewandowski wanaona ni kujichimbia
kaburi zaidi.
United
wana amini kuwa endapo nyota hao watatua Old Traford itakuwa changamoto
kubwa kwa Mholanzi Robin Van Persie ambaye atakuwa anakamilisha miaka
30 akiwa na malengo ya kutetea ubingw wake alioutwaa msimu uliopita.
Bunduki
mbili za ukweli: Man United wana imani kubwa ya kuwanasa washambuliaji
wawili kwa mpigo, Cesc Fabregas (juu) na Robert Lewandowski (chini)
Robert Lewandowski
Changamoto
mpya: Robin van Persie atapata changamoto kubwa katika nafasi yake ya
ushambuliaji baada ya mashine hizo kuzama Old Traford
Anasemekana
kuondoka, Wayne Rooney amekuwa akihusihwa kuondoka United na kujiunga
na Arsenal, endapo atabaki United, itakuwa ngumu sana kupata namba baada
ya mashine mpya kutinga
0 comments:
Post a Comment