Miss Sinza 2012-2013, Brigitte Alfred (kushoto) akimvisha Taji Redd’s Miss Sinza 2013, Prisca Element, baada ya kutangazwa mshindi wa taji hilo katika shindano lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye Ukumbi wa Meeda Club, Sinza jijini Dar es Salaam.
Redd’s
Miss Sinza 2013, Prisca Element (katikati) akiwa na Mshindi wa pili
Happynes Maira (kulia) na Mshindi wa tatu, Sarahy Paul, wakiwa na furaha
mara baada ya kutangazwa washindi katika shindano lao lililokuwa
likishikiliwa na Redd’s Miss Sinza na Miss Tanzania 2012-2013, Brigitte
Alfred.
Warembo wa Redd’s Miss Sinza, wakicheza shoo ya ufunguzi wa shindano lao.
********************************************
Na www.sufianimafoto.com
Prisca
Element usiku wa kuamkia leo alitwaa taji la mrembo wa Redds Miss Sinza
2013 katika kinyang’anyiro kilichowashirikishwa jumla ya warembo 12,
kwenye ukumbi wa Meeda Club na kurithi taji la kwanza la Redds Miss
Tanzania, Brigitte Alfred.
Haikuwa
kazi rahisi kwa Prisca kutwaa taji hilo kutokana na ushindani mkubwa
kutoka kwa warembo bora 11 walioshiriki mashindano hayo yaliyodhaminiwa
na Redds Original, Dodoma Wine, Fredito Entertainment, Chilly Willy
Energy Drink, Sufiani Mafoto blog, Salut5 na CXC Africa.
Hata
hivyo, Prisca aliweza kuwazidi kete wanzake na kutwaa taji hilo
sambamba na zawadi ya Kitita cha Sh. 400,000 zilizotolewa na waandaaji
wa mashindano hayo Calapy Entertainment chini ya ukurugenzi wa Majuto
Omary.
Mwenyekiti
wa Serikali ya Mtaa wa Sinza A, Juma Mgendwa alikabidhi zawadi hiyo kwa
Prisca ambaye alisema kuwa amefurahi kushinda taji hilo na kazi yake
kubwa ni kutwaa taji la Miss Kinondoni.
“Kwangu ni historia kutokana na ukweli kuwa nimerithi taji la Redds Miss Tanzania Brigitte Alfred, na ninaahidi kufanya kweli katika mashindano yanayofuata na kutwaa mataji ya Miss Kinondoni na vile vile taji la Redds Miss Tanzania, nitashirikiana na waandaji wangu ili kufanya maandalizi ya kina ili kufikia malengo hayo,” alisema Prisca.
“Kwangu ni historia kutokana na ukweli kuwa nimerithi taji la Redds Miss Tanzania Brigitte Alfred, na ninaahidi kufanya kweli katika mashindano yanayofuata na kutwaa mataji ya Miss Kinondoni na vile vile taji la Redds Miss Tanzania, nitashirikiana na waandaji wangu ili kufanya maandalizi ya kina ili kufikia malengo hayo,” alisema Prisca.
Nafasi
ya pili ilichukuliwa na Happiness Maira ambaye alizawadiwa sh. 300,000
alizokabidhiwa na Mratibu wa Masoko na Biashara wa kinywaji cha Dodoma
Wine, Frank Matonda na zawadi ya mshindi wa tatu ilikwenda kwa Sarahy
Paul na kukabidhiwa zawadi ya shs 200,000 na Swabir Abdulrehman ambaye
ni Mkurugenzi wa Usambazi wa Kampuni ya TSN Distribution kupitia
kinywaji cha Chilly Willy.
Nafasi
ya nne ilichukuliwa na Nicole Michael na tano ilichukuliwa na Nasra
Hassan ambao wote walizawadiwa shs 150,000 kila mmoja na Mkurugenzi wa
Mashindano hayo, Majuto. Warembo hao watano wataiwakilisha Sinza katika
mashindano ya Miss Kinondoni 2013.
Mashindano
hayo yalishuhudiwa na umati mkubwa wa mashabiki wa urembo na kupambwa
na burudani safi ya bendi bora nchini, African Stars maarufu kwa jina la
Twanga Pepeta ambayo ilitambulisha baadhi ya nyimbo zake mpya za albamu
ya Nyumbani ni Nyumbani.Twanga Pepeta ilifanya mambo makubwa jukwaani
huku ikiwa ikitumbuiza kwa mara ya kwanza kwa kipindi cha mwaka mmoja na
zaidi.
Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga (katikati) akiwa
na Albert Makoye (kushoto) na Miss Tanzania 2013, Brigitte Alfred,
wakishuhudia shindano hilo.
Shoo ya utangulizi ikiendelea…
0 comments:
Post a Comment