Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Kocha
mpya wa mashetani wekundu, Manchester United wenye makazi yao katika
dimba la Old Traford jijini Manchester, nchini England, David Moyes
ameweka wazi nini anataka wachezaji wake na wasaidizi wake wafanye mara
atakapoanza kibarua cha kusuka mashine zake kwa ajili ya kutetetea
ubingwa wa ligi kuu na michaono ya ligi ya mabingwa barani ulaya msimu
ujao.
Kocha
huyo wa zamani wa klabu ya Everton amesema kazi yake ya kwanza ni
kujitafutaia heshima katika kikosi cha United na klabu nzima kwa ujumla.
Moyes
ambaye amerithi mikoba ya Sir Alex Ferguson na kutarajiwa kuanza kazi
julai mosi mwaka huu tayari ameanza kazi nyuma ya pazia.
“Kama
unataka kufanya kazi na mimi, unatakiwa kukubali kufanya kazi siku saba
za wiki. Nahitaji wafanyakazi wangu kujua hilo, nahitaji jitihada zao
kwa hilo”. Alisema Moyes.
Pia
aliongeza kuwa wachezaji lazima wawe na nidhamu kubwa, huku akiweka wazi
kuwa katika kikos chake anatarajia kuwapa nafasi zaidi vijana.
Moyes amesema anataka kujenga heshima kubwa katika klabu yake kubwa ya Manchester United
Je, ataweza kulinda heshima ya Sir Alex Ferguson pale United?
Viatu vizito kavaa: Moyes atakiongoza kikosi cha United kutetea ubingwa wake katika msimu wa 2013-14
0 comments:
Post a Comment