Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Kocha
mwenye jina kubwa na maneno mengi Mreno Jose Mario Dos Santos Mourinho
Ferlix amethibitisha rasmi kuwa mwishoni mwa wiki hii atakuwa kocha wa
wazee wa London, Chelsea baada ya kutimka Real Madrid wikiendi
iliyopita.
“Naelekea London leo jumatatu na mwishoni mwa wiki hii nitakuwa kocha wa Chelsea”. Mourinho ameiambia Televisheni ya Spanish TV.
Mourinho
alisisitiza kuwa mashabiki wa Chelsea na viongozi wa klabu hiyo
wanampenda sana na ukiwa binadamu lazima uangalie hilo katika maisha.
Kocha
huyo alisema maisha ni mazuri lakini mafupi, hivyo unatakiwa kufanya
kile unachodhani ni kizuri, na ndio maana anarejea Chelsea.
Mourinho
aliingoza klabu yake katika mechi ya mwisho ya La Liga dhidi ya Osasuna
ambapo walishinda mabao 4-2 na sasa yuko njiana kuenda zake kwa bosi
wake Roman Abramovich, mmiliki wa Chelsea mabaye walitibuana mwaka 2006.
Anarudi England: Jose Mourinho anarudi zake London leo hii na kukamilisha maneno ya watu kuwa anarudi Chelsea
Kwaheri
Santiago Bernabeu: Jose Mourinho katika mchezo wake wa Mwisho wa ligi
kuu nchini Hispania kabla ya kurejea England kuwa kocha mkuu wa Chelsea.
Mawazo
mchanganyiko: Baadhi ya mashabiki wa Madrid walimshukuru Mourinho
wakati wengine walisema hawataki kumuona tena katika maisha yao’
0 comments:
Post a Comment