IMEWEKWA JUNI 24, SAA 11:59 ASUBUHI
MSHINDI
wa tuzo ya utunzi bora wa nyimbo za bongo fleva ya Kili Music mwaka
huu, Ben Paul amethibitisha na kukamilisha taratibu zote za kutumbuiza
katika shindano la kanda ya Temeke, litakalofanyika Julai 5, katika
ukumbi wa TCC Club Chang’ombe.
Ben
Paul ambaye ni kipenzi cha mashabiki warembo kwa sasa, akiwa anatamba
na nyimbo lukuki zikiwemo Pete, Yatakwisha, Nikikupata na Waubani,
atakuwa sambamba na bendi ya The African Stars “Twanga Pepeta”, ambao
itakuwa ni mara tu baada ya kuzindua albamu ya 13.
Shindano
la Redds Miss Temeke, litakuwa linafanyika siku chache tu kabla ya
mfungo wa Ramadhan, hivyo ni kama vunja jungu kwa wale wataoingia katika
mfungo. Warembo 16 wamekuwa wakiendelea na mazoezi chini ya wakufunzi
Suzan Mwenda na Shadya Mohamed.
Warembo
hao ni pamoja na Aksaritha Vedastus ,Irene Rajab, Darline Mmary,
Esther Muswa Hyness Oscar, Latifa Mohamed, Jamila Thomas, Margreth
Rajab, Magdalena Olotu, Mey Karume,Mutesa George, Naima Ramadhan,
Narietha Boniface, Stella Mngazija na Svtlona Nyameyo.
Mashindano
hayo yamedhaminiwa na Redds Original, Dodoma Wine, CXC Africa, City
Sports Lounge, Blogu ya Wananchi, RIO Quality Gym &Spa, Fredito
Entertainment na Kitwe General Traders. Temeke, imewahi kutoa warembo
kadhaa miaka ya nyuma waliopata mafanikio katika mashindano hayo,
mitindo na kazi nyingine hasa kupata uzoefu wa kujiamini katika njanja
mbalimbali.
Miongoni
mwao ni Miriam Odemba(1997) aliyepata kuiwakilisha Tanzani katika
fainali za mitindo zilizofanyika Nice Ufaransa na kupata mkataba wa
Elite Model Look, baadaye kufakinikiwa kutwaa nafasi ya pili ya Miss
Earth World, zilizofanyika China.
Pia,
Temeke ilimtoa Happines Millen Magesse(2001), na kutwaa taji la Miss
Tanzania na kwa sasa anang’ara sana katika tasnia ya mitindo katika nchi
za Marekani, Afrika Kusini na barani Afrika kwa ujumla. 2003 Temeke
ilimtoa Miss Tanzania, Sylvia Bahame na 2006 kuwatoa Jokate Mwegelo na
Irene Uwoya.
Jokate
alitwaa taji la Miss Temeke mwaka huu na pia kushika nafasi ya pili
Miss Tanzania na pia kushinda taji la ubalozi wa Redd’s na gazeti la
Citizen. Uwoya ambaye alikuwa mshindi wa pili Temeke alishika nafasi ya
nne kwenye Miss Tanzania mwaka huo. Genevieve Mpangala mwaka 2010
alitwaa taji la Miss Temeke baadaye kushinda taji la Miss Tanzania.
Nafasi
nyingine za juu zilizowahi kutwaliwa na warembo kutoka Temeke ni pamoja
na Irene Kiwia, mshindi wa nne Miss Tanzania mwaka 2000, Regina Mosha
mshindi wa nne Miss Tanzania mwaka 2002, Cecylia Assey mshindi wa pili
Miss Tanzania 2004, Queen David mshindi wa tatu mwaka 2007 na Edda
Sylvester mshindi wa tatu Miss Tanzania akiwa anashikilia taji la Redds
Miss Temeke
0 comments:
Post a Comment