Sunday, June 16, 2013

soccer-morocco
Na Baraka Mpenja
JANA kulikuwa na Mechi kadhaa za Makundi Barani Afrika kusaka Timu 5 zitakazocheza Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil Mwaka 2014 na zifuatazo ni taarifa fupi ya baadhi ya Mechi hizo.
Morocco 2 Gambia 0
Morocco Jana waliipikua Tanzania Nafasi ya Pili ya KUNDI C baada ya kuichapa Timu ya mkiani Gambia kwa Bao 2-0 katika Mechi iliyochezwa huko Marrakech.
Bao za Morocco zilifungwa na Barrada na Younes Belhanda.
Katika KUNDI C, ambalo leo, Tanzania inaikaribisha Ivory Coast Jijini Dar es Salaam, Ivory Coast ndio Vinara wakiwa na Pointi 10, Morocco 8, Tanzania 6 na Gambia 1.
Uganda 2 Angola 1
STRAIKA wa Uganda, Emmanel Okwi Jana aliifungia Uganda Bao muhimu katika Mechi yao ya KUNDI J la kuwania kwenda Brazil Mwaka 2014 kucheza Fainali za Kombe la Dunia walipoifunga Angola Bao 2-1 na kutwaa uongozi wa Kundi hilo.
Katika Mechi hiyo, Angola walitangulia kufunga kupitia Job lakini Uganda walipiga Bao 2 Wafungaji wakiwa Emmanuel Okw na Tonny Mawejje.
Ushindi huo umewafanya Uganda wawe juu ya Senegal kwa Pointi 2 na leo huko Monrovia Lineria itacheza na Senegal.
Congo 0 Burkina Faso 1
Kwenye KUNDI E, waliokuwa Vinara, Congo wakiwa Nyumbani Pointe Noire, walijikuta wakipoteza uongozi huo kwa kuchapwa Bao 1-0 na Burkina Faso kwa Bao la Aristide Bance na sasa Burkina Faso wako kileleni Pointi 2 mbele ya Congo.
Burkina Faso ndio walimaliza wa pili nyuma ya Mabingwa Nigeria kwenye AFCON 2013.
Katika Mechi nyingine ya KUNDI E, Hetitriki ya Pierre-Emerick Aubameyang iliwapa ushindi wa Bao 4-1 Gabon dhidi ya Niger na kuwa Pointi 2 nyuma ya Vinara Burkina Faso.
Zambia 1 Sudan 1
Wakiwa kwao, Zambia jana walibanwa na kutoka Sare ya Bao 1-1 na Sudan ambayo haina matumaini ya kusonga mbele.
Matokeo hayo yamewafanya leo Ghana, ambao wako Ugenini kucheza na Lesotho, kuwa na nafasi murua kutwaa uongozi wa KUNDI D ikiwa watashinda na kujiweka kwenye hali nzuri kucheza na Zambia huko Accra katika Mechi yao ya mwisho ya Kundi.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video