Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akizungumza na waumuni wa
kanisa katoliki Emaus Centre Ubungo Jijini Dar walioshiriki katika ibada
ya kupanda mbegu hivi karibuni. Mkuu huyo wa Mkoa alialikwa kama mgeni
rasmi kuongoza zoezi hilo la kupanda mbegu ambalo lilifanikiwa kukusanya
Tsh. Milioni 41.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akizungumza na waumuni wa
kanisa katoliki Emaus Centre Ubungo Jijini Dar es Salaam ambapo
aliwaasa juu ya umuhimu wa kutunza amani iliyopo nchini kwa kujiepusha
na mambo madogomadogo yanayoweza kuondoa amani iliyopo ikiwemo mijadala
ya kuchinja ambayo ilishaanza kufanya machafuko nchini. Hata hivyo
aliwaomba waumini hao kuwaombea wanasiasa wafanye kazi zao vizuri kwa
haki, usawa na uwajibikaji badala ya kuishia kuwatupia lawama ambazo
hazijengi.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akishiriki kukusanya sadaka
zilizokuwa zikitolewa na waumini wa kanisa katoliki Emaus Centre Ubungo
Jijini Dar walioshiriki katika ibada ya kupanda mbegu hivi karibuni.
Mkuu huyo wa Mkoa alialikwa kama mgeni rasmi kuongoza zoezi hilo la
kupanda mbegu ambalo lilifanikiwa kukusanya Tsh. Milioni 41.
Waumini
wa kanisa katoliki kutoka sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam
waliokuwa wamekusanyika “Emaus Centre” Ubungo kwa ajili ya ibada ya
kupanda mbegu iliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella
Manyanya hivi karibuni.
(Picha na Hamza Temba)
0 comments:
Post a Comment