Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na Mke wa Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa Mama Ban Soon-Taek wakati wa hafla ya chakula cha
mchana kilichoandaliwa na mke wa Waziri Mkuu wa Japan Mama Akie Abe
kwenye hoteli ya New Grand huko Yokohama nchini Japan tarehe 2.6.2013.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na Mke wa Waziri Mkuu wa Japan
Mama Akie Abe (kushoto) na Mke wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mama
Moon Soon-Taek (katikati) wakati wa chakula cha mchana ambacho Mama Abe
aliwaandalia wake wa Marais na wakuu wa nchi za Afrika wanaohudhuria
mkutano wa -Tokyo International Conference on African Development-TICAD V
unaofanyika huko Yokohama nchini Japan tarehe 1-3.6.2013
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na Mama Lordina Mahama, Mke wa Rais
wa Ghana (kushoto) na Mama Ban Soon-Taek wakati wa chakula cha mchana
kilichoandaliwa na Mke wa Waziri Mkuu wa Japan Mama Akie Abe kwenye
hoteli ya New Grand huko Yokohama nchini Japan tarehe 2.6.2013.
Baada
ya kupata chakula cha mchana wake wa Marais na wakuu wan chi za Africa
wanaonekana wakibadilishana mawazo. Pichani ni Mama Lordina Mahama,
Mama Salma Kikwete, Mama Moon Soon-Taek na Mama Sia Nyama Koroma, mke wa
Rais wa Sierra Leone Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akijumuika na wake wa Marais na wakuu wa
nchi za Afrika wakiangalia maonyesho ya traditional calligraphy
yaliyokuwa yakionyeshwa na wanafunzi mara baada ya chakula cha mchana.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na wanafunzi wa high school
baada ya wanafunzi hao kufanya maonyesho ya traditional calligraphy
katika hoteli ya New Grand mjini Yokohama tarehe 2.6.2013. Mwenyekiti
wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akiaagana
na Mama Akie Abe, mke wa Waziri Mkuu wa Japan mara baada ya chakula cha
mchana. Katikati ni Mke wa Rais wa Mali Mama Traore Mentou Doucouri.
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama
Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mke wa Waziri Mkuu wa
Japan Mama Akie Abe (wa kwanza kushoto) na wa pili ni mke wa Rais wa
Namibia Mama Penekupifo Pohamba wakati wa chakula cha mchana huko
Yokohama tarehe 2.6.2013.
PICHA NA JOHN LUKUWI.
0 comments:
Post a Comment