Mahmoud Ahmad Arusha
Uchaguzi
wa udiwani kwenye jimbo la Arusha umechukuwa sura mpya baada ya mgombea
wa udiwani wa chama cha wananchi (CUF)kwenye kata ya Elerai John
Gilbert Bayo kuangua kilio jukwaani wakati akinadi sera zake mbele ya
wananchi, wakazi wa kata hiyo na katibu mkuu wa chama hicho Maalim Seif
Sharif Hamad.
Mgombea
huyo aliangua kilio hicho baada ya kuwaambia na kuapa mbele ya wakazi
hao wa kata yake kuwa hakuwahi kupokea fedha kiasi cha 50 milion kwa
ajili ya kupata muafaka wa meye wa jiji la Arusha kama chama cha
demokrasia na maendeleo wanavyodai na kuwa hata weza kukiuka maadili na
kuwatosa waliomchagua.
Akizungumza
kwenye kampeni hizo katibu mkuu wa CUF na makamu wa kwanza wa serikali
ya umoja wa kitaifa ya Zanzibar Seif Sharif Hamad aliwataka wakazi wa
kata ya Elerai kuwachagua wagombea wa chama hicho kwani chama hicho
kimekuwa kikihimiza umoja na Amani wakati wote.
Maalimu
Seif akabainisha kuwa Mgombea wa CUF kwenye kata ya Elerai John Bayo ni
mtu makini na mchapakazi na kuwa wao hawapo kumfukuza mtu bali wananchi
ndio watakao amua hatma ya viongozi wanaowataka kwani sisi CUF ndio
walimu wa amani hapa nchini kama tungekuwa hatuhubiri amani Zanzibar
isinge kalika baada ya uchaguzi mkuu kwani chaguzi zote tuliweza
kushinda lakini tulipokwa ushindi.
“Sisi
CUF ndio wahubiri wa amani kwani tangu mwaka 1995 tumeshinda chaguzi
zote lakini kwa hekima na busara tuliwakataza vijana kuingia barabarani
kudai haki yao lakini leo matunda ya busara si mnayaona”alisema Maalimu
Seif.
Zanzibar
wananchi waliishi kwa uhasama na tukaona kama tutaenda hivyo kwenye
uchaguzi wa mwaka 2010 basi kutaweza kutokea mchafuko hivyo mimi na Rais
mstaafu Karume tulikaa na baaadae vyama na hatimaye wananchi zaidi ya
66%akaidhinisha muafaka huu ni uamuzi wa busara na leo ndiyo iliyozaa
serkali ya umoja wa kitaifa.
Maalimu
akatanabaisha kuwa CUF inaimani na John Bayo kwa kuwa ndiyo chaguo la
wananchi wa kata hiyo na kuwataka kumpa kura zote ili awe diwani wao na
kusema hivi sasa Zanzibar imetulia baada ya mwafaka ule na haya ni
matunda ya chama hicho na kuwa hawatajuta kuchagua mgombea wa chama
hicho kwenye kata zote waliosuimamisha wagombea.
Naye mgombea wa udiwani wa Kata ya Elerai John Bayo
alisema
kuwa akichaguliwa atapambana na kero mbalimbali zinazowakabili wakazi
wa kata hiyo ikiwemo kutoa michango ya kununua madawati na majembe kila
mwaka kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.
Bayo
akawataka wakazi wa kata hiyo kuwaonyesha kuwa hakuchaguliwa na mafuriko
ya Chadema kwa kumpigia kura ya ndiyo kwenye uchaguzi huo siku ya
tarehe 16 mwezi huu na kuwa majengo ya Zahanati wao hawataki zahanati
bali kituo cha Afya hivyo wakimpa ridhaa kero hizo ndiyozitakuwa kipaumbele chake.
0 comments:
Post a Comment