Na Baraka Mpenja
Haya
sasa, ukiona moshi ujue kuna kitu kimechomwa!!, Maafande wa jeshi la
kujenga taifa wa mkoani Tanga “waja leo waondoka leo”, Mgambo Shooting
wanatarajia kutangaza kikosi chao kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu
soka Tanzania bara kesho kutwa mjini Tanga.
Matandao wa MATUKIO DUNIANI umekutana na katibu mkuu wa klabu hiyo bwana Antony Mgaya akiwa katika
kona zake na kueleza kuwa ijumaa ya wiki hii watatangaza kikosi chao kwa
maana ya wachezaji waliowasajili na kuachwa kwa ajili ya msimu ujao
unaotarajia kuanza kutimua vumbi mwezi Agosti mwaka huu.
“Sisi
mambo yetu ni kimya kimya tofauti na Simba na Yanga ambao mambo yao
yanajaa kwenye vyombo vya habari, lakini niseme kitu kimoja kuwa,
viongozi wametulia na kutafuta wachezaji wazuri kufuatana na
mapendekezo ya kocha wetu , Mohamed Kampira. Majina yote yataanikwa
wiki hii na mashabiki wetu wakae mkao wa kula”. Alisema Mgaya.
Mgaya
alisema katika kikosi chao hakuna mchezaji mkongwe sana, wamesajili
wachezaji ambao hawana majina, lakini viwango vyao ni hatari sana.
Katibu
huyo alisema baada ya kutangaza majina ya wachezaji wao siku hiyo, wiki
ijayo jumatatu wataingia rasmi kambini kuanza mawindo ya msimu wa ligi
kuu wa 2013/2014.
“Tunataka
jumatatu tuingie kambini, bora kuwahi kujipanga, tumejifunza mengi
msimu uliopita, sasa hatutaki kufanya makosa hata kidogo, lazima
tujiandae mapema ili kuleta ushindani mkubwa zaidi”. Alisema Mgaya.
Mgaya
alisema wamekaa na kufanya tathmini kubwa na kugundua kuwa msimu wao wa
kwanza ulikuwa mgumu sana kwao, lakini kwa sasa wanajua nini cha
kufanya na lazima washindane vilivyo msimu ujao.
“Tulinusurika
sana ndugu yangu, hakika tulihaha sana. Ule wakati wa mahangaiko
umekwisha kwani tumejifunza mengi, waswahili husema makosa ni shule.
Nafikiri kwa sasa tutakuwa vizuri sana”. Alisema Mgaya.
0 comments:
Post a Comment