Sunday, June 16, 2013

SIMB 
Mfaransa, Patrick Liewig (kulia) akizungumza na msaidizi wake Jamhuri Kiwhelu “Julio”

Na Baraka Mpenja
Aliyekuwa kocha wa wekundu wa msimbazi Simba, Mfaransa Patrick Liewig ameendelea kusisitiza nia yake ya kuwaburuza Simba mahakamani endapo watapuuzia haki yake ya msingi katika mkataba wake na klabu hiyo.
Katika mahojiano maalumu, Liewig ameimbia MATUKIO DUNIANI kuwa anaheshimu sana maamuzi ya Simba kumuachisha kazi yake ya kukinoa kikosi chake, lakini nao waheshimu makubaliano ya mkataba wake ambao unaisha mwakani mwezi wa sita.
“Mimi sikuambiwa kama nimefukuzwa bali niliambiwa nikapumzike, nimerudi kuifundisha timu yangu kujiandaa na Kombe la Kagame, nimekuja na mipango yangu ya mazaoezi, nafika nakuta Simba wameajiri kocha mpya, sawa naheshimu maamuzi yao lakini nao waheshimu mkataba”. Alisema Liewig.
Kocha huyo aliyemaliza ligi akiwa nafasi ya tatu katika msimamo na mbaya zaidi akafungwa na Ynaga mabao 2-0 mechi ya mwisho ya ligi kuu soka Tanzania bara mei 18 mwaka huu, amesisitiza kuwa yeye anajitambua kuwa ni kocha wa simba na ana mkataba ambao unaisha mwezi juni mwakani, na kama Simba wameamua kuuvunja sawa, lakini wanatakiwa kumlipa madai yake ili atimke zake nchini.
“Mimi nashangaa sana, kwanini wasingeniambia mapema kuwa hawanitaki, naipenda kazi yangu na mimi ni kocha wa kimataifa, wachezaji walikuwa wanashindwa kunielewa mwanzoni, lakini ikafika wakati wakanipatia vizuri, nimekuja kuisaidia timu halafu nakutana na hali hii, imenichosha sana.” Alisema Liewig.
Liewig maarufu kama “Babu” alisisitiza kuwa kwa sasa anawasiliana na mwanasheria wake ili kudai haki zake za msingi, na kamwe Simba wasijisumbue kwani lazima wamlipe madai yake ya mkataba.
Kwa sasa kocha Abdalaah Kibadeni “King Mputa” amerithi mikoba ya Liewig na tayari ameshaanza kazi rasmi Msimbazi.
MATUKIO DUNIAN ilihitaji kujua kama Liewig anaweza kufundisha timu nyingine ya soka nchini Tanzania endapo akipata nafasi, na ndipo alipojibu kuwa anaweza kufundisha, lakini akasema timu anazoweza kufundisha ni Azam fc au Yanga.
“Naweza kufundisha timu nyingine kama Azam na Yanga, lakini sidhani kama naweza kupata nafasi kwani tayari Yanga ni mabingwa na wanamuamini kocha wao, hali kadhalika Azam fc wanaendelea vizuri na kocha wao, hivyo sina imani ya kupata nafasi katika timu hizo”.Alisema Liewig.
Kocha huyo aliongeza kuw amefurahi kuwaona vijana wake wakiendelea vizuri katika kikosi cha Taifa Stars ambapo alifurahi zaidi kumuona adui yake Mwinyi kazimoto Mwitula akipasha misuli katika kikosi cha stars.
“Nimefurahi kumuona Mwinyi, tuligombana sana na mimi, kama nisingefanya vile usingekuwepo hapa leo hii, nimefurahi amekuja kunisalimia, nampenda sana”. Alisema Liewig.
Akizungumzia mchezo wa leo katika ya taifa stars dhidi ya Ivory Coast, Liewig amesema Taifa stars wanaweza kupata ushindi kama wachezaji watajituma na kusikiliza maelezo ya mwalimu.
Kocha huyo alisema Ivory coast anawafahamu vizuri na wana wachezaji bora zaidi, lakini katika soka wanaweza kufungwa vizuri tu.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video