Na Baraka Mpenja
Ikiwa
katika harakati za kujenga timu ya muda mrefu, klabu mpya ya ligi kuu
soka Tanzania bara msimu ujao, Mbeya City ya jijini Mbeya anaendelea na
mpango wake wa kuandaa kikosi cha pili cha klabu hiyo kwa lengo la kuwa
na timu ya ushindani kitaifa na kimataifa.
Kocha msaidizi wa klabu hiyo inayonolewa na kocha Juma Mwambusi, Mwalimu Maka Mwalwisyi ameimabia MATUKIO DUNIANI
kuwa kwa sasa wanaendelea na mazozezi ya kikosi cha pili ambacho
kimeteuliwa na benchi la ufundi la klabu hiyo, wakati viongozi wa timu
wakiweka mambo safi ili timu A iingeia kambini kujiandaa na michuano ya
ligi kuu msimu ujao.
“Tunataka
kuijenga falsafa ya Mbeya City, kufanikisha hilo tunahitaji kuwa na
timu bora ya vijana ambao tutakuwa tunawapandisha timu A. Kwasasa tupo
na vijana wengi sana, tunajaribu kuchambua wanaotufaa ili kupata timu ya
chini ya umri wa miaka 20”. Alisema Mwalwisyi.
Kocha huyo alisema kuwa wachezaji wao wanaonesha juhudi kubwa ya kujifunza, jambo ambalo linatia matumaini kwa benchi la ufundi.
“Vijana
wana vipaji vya hali ya juu. Wanacheza kwa kujituma sana, mbali na hayo
wana nidhamu ya mazoezi, wanazingatia sana maelekezo ya waalimu wao”.
Alisema Mwalwisyi.
Mwalwisyi alisisitiza kuwa malengo yao ni kuifanya Mbeya City kuwa klabu ya ushindani mkubwa na sio washiriki wa ligi kuu bara.
Aidha
alisema katika kuhakikisha hilo, benchi la ufundi linataka kuwekeza
katika soka la vijana ambao ndio chagua sahihi kwa soka la sasa.
“Soka
la kisasa kwa kweli linahitaji sana vijana ambao wanaenda sambamba na
kasi ya mpira wa dunia, kwa kulijua hilo, Mbeya City lazima iwe kitalu
cha kuzalisha wachezaji wa Tanzania”. Alisema Mwalwisyi.
Pia
kocha huyo aliwataka mashabiki wa Mbeya kuwaunga mkono wao na ndugu zao
Tanzania Prisons, wawakilishi wa jiji la Mbeya michuano ya ligi ya
Premia ya Tanzania bara.
0 comments:
Post a Comment