Na Baraka Mpenja
Kikosi
cha pili cha klabu mpya ya ligi kuu soka Tanzania bara, Mbeya City ya
jijini Mbeya kinatarajia kushiriki michuano ya Kombe la Muungano
litakalofanyika Mufindi kijiji cha Igolole mkoani Iringa.
Kocha msaidizi wa kikosi hicho kinachonolewa na mwalimu Juma Mwambusi, Mwalimu Maka Mwalwisyi ameimbia MATUKIO DUNIANI kuwa wataanza kutupa karata yao ya kwanza mnamo juni 30 mwaka huu.
“Mwaka
huu tumechelewa sana kuanza michuano hii, udhamini umeelezwa kuwa
tatizo, lakini wasimamizi wametuambia kuwa mambo yanakwenda vizuri na
hapo juni 30 tutaanza kampeni yetu”. Alisema Mwalwisyi.
Mwalwisyi
alisema mazoezi hayo ya kikosi cha pili ni njia mojawapo inayotumiwa na
benchi la ufundi kuhakikisha wanapata wachezaji wa kuwapandisha kikosi
cha kwanza kitakachoshiriki ligi kuu soka Tanzania bara msimu ujao.
Kocha huyo alisema vijana wao wana morali kubwa ya kushiriki michuano ya Muungano na wameahidi kuibuka mabingwa kwa mwaka huu.
“Kizuri
tunaenda sanjari na watani wetu wa jadi , Mbaspo Academy, ni wakati
muafaka kwetu kujidhihirishia ufalme wa soka nyanda za juu kusini,
tunajipanga vizuri sana kuhakikisha tunafanya vizuri sana”. Alisema
Mwalwisyi.
Kuhusiana
na kikosi cha kwanza kuanza mazoezi kwa ajili ya ligi kuu, kocha huyo
alisema taratibu zote zimekamilika, wanasubiri tu uongozi useme kuhusu
hilo na wao benchi la ufundi waanze kupiga mazoezi ya kufa mtu.
Mwalwisyi
aliwataka mashabiki wa soka mkoani Mbeya kuwaunga mkono sana kipindi
hiki kipya cha klabu hiyo kwani soka linachezwa uwanjani na nje ya
uwanja ambao sapoti ya wadau na mashabiki inachangia sana kupata
mafanikio.
0 comments:
Post a Comment