Mjumbe
wa halmashauri kuu CCM (NEC) manispaa ya Singida, Hassan Mazala
akizungumza juzi kwenye halfa ya uzinduzi wa hotel ya ya Chemuchemu park
na shina la wakereketwa wa CCM wa hoteli hiyo mpya.
Mfanyabiashara
maarufu mjini Singida, Mushi Kimboka (aliyweshika maiki) akitoa taarifa
yake kwa mjumbe wa halmashauri kuu CCM (NEC) taifa manispaa ya Singida,
Hassan Mazala(aliyevaa miwani) juu ya ujenzi wake wa hotel ya
Chemuchemu Park iliyoko katika kijiji cha Manguanjuki nje kidogo ya mji
wa Singida.
Mkurugenzi
mtendaji wa hotel ya kitalii ya Stanley Motel, Eward Malya maarufu kwa
jina la Hali Ngumu akitoa nasaha zake kwenye hafla ya uzinduzi wa hotel
ya Chemuchemu park iliyopo kijiji cha Manguanjuki nje kidogo ya mji wa
Singida.Hali Ngumu amewataka wafanyabiashara kufanya biashara halali kwa
bidii na kisha wabane matumizi kwa madai kuwa ‘hali ni ngumu’.
Mjumbe
wa halmashauri kuu CCM (NEC) taifa manispaa ya Singida,Hassan Mazala
akizindua rasmi hotel ya Chemuchemu Park iliyopo katika kijiji cha
Manguanjuki nje kidogo ya mji wa Singida.
Wanachama
wapya wa CCM baada ya kukabidhiwa kadi juzi na mjumbe wa halmashauri
kuu CCM (NEC) taifa Hassan Mazala (hayupo kwenye picha).
Kikundi
cha burudani cha kijiji cha Manguanjuki kikitoa burudani wakati wa
uzinduzi wa shina la wakereketwa wa CCM katika hotel ya Chemuchemu park.
Mjumbe
wa halmashauri kuu CCM (NEC) taifa manispaa ya Singida,Hassan Mazala
(wa tano kushoto mbele) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau
waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa hotel ya Chemuchemu park iliypo
kijiji cha Manguanjuki nje kidogo ya mji wa Singida.(Picha zote na
Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu.
Mjumbe
wa halmashauri kuu ya CCM (NEC) taifa manispaa ya Singida Hassan
Mazala, amewahimiza wafanyabiashara wa ngazi zote kujiunga na CCM, kwa
madai kuwa ni chama pekee kinachowajengea mazingira mazuri ya kufanya
shughuli zao kwa amani na utulivu.
Mazala ametoa wito huo muda mfupi baada ya kuzindua tawi la wakereketwa
wa hotel mpya na ya kisasa ya Chemuchemu Park, iliyopo katika kijiji cha
Manguanjuki nje kidogo ya mji wa Singida.
Amesema uzoefu unaonyesha wazi kwamba wafanyabiashara wamekuwa
wakishirikiana na CCM kwa muda mrefu na hali hiyo inapaswa kuendelezwa
kwa sababu inazinufaisha pande zote mbili.
Akifafanua zaidi amesema amani na utulivu ndio inayopelekea
wafanyabiashara na Watanzania wengine wote, wafanye shughuli zao halali
kwa uhuru mpana zaidi na ambao hauathiri sheria zilizowekwa.
MNEC
huyo amesema CHADEMA inaonyesha ilani yake ni kupandikiza chuki,
hasira, kuchonganisha watu na upotoshaji uliopitiliza, na kwa hali hiyo,
CHADEMA sio mahali rafiki kwa wafanyabiashara.
Katika hatua nyingine, Mazala ametumia fursa hiyo kuwahimiza
viongozi/watendaji wa CCM na wa serikali yake, kuwa karibu na
wafanyabiashara ili kujua matatizo/kero wanazokabiliana nazo na
kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu.
Kwa upande wa wafanyabiashara, amewataka wafanye kazi halali kwa bidii
na kwa ubunifu mkubwa na kuhakikisha wanabana matumizi au wawe na
nidhamu ya matumizi.
0 comments:
Post a Comment