Nahodha
wa timu ya Makumbusho United Hamza Mohamed akipokea kombe la ubingwa wa
Airtel Rising Stars, mkoa wa Kinondoni, kutoka kwa Ofisa Maendeleo wa
TFF Bw. Salum Madadi baada ya kuibamiza timu ya Mtakuja 5-1 katika
mchezo wa mwisho wa mashindano ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka
17 uliofanyika kwenye uwanja wa Mwanyamala shule ya msingi jijini Dar es
Salaam leo Juni 25, 2013.
Nahodha
wa timu ya Makumbusho United Hamza Mohamed akinyanua juu kombe la
ubingwa wa Airtel Rising Stars, mkoa wa Kinondoni, baada ya kuibamiza
timu ya Mtakuja 5-1 katika fainali ya mashindano hayo ngazi ya mkoa
iliofanyika kwenye uwanja wa Mwanyamala shule ya msingi jijini Dar es
Salaam leo Juni 25, 2013.
Wachezaji
wa timu ya Makumbusho United wakishangilia baada ya kutwaa kombe la
ubingwa wa Airtel Rising Stars, mkoa wa Kinondoni, kwenye uwanja wa
Mwanyamala shule ya msingi jijini Dar es Salaam leo Juni 25, 2013.
Makumbusho walishinda 5-1 dhidi ya Mtakuja.
…………………………………………………………………
Timu
ya Makumbusho United imetawazwa kuwa mabingwa wa Airtel Rising Stars
mkoa wa kisoka wa Kinondoni baada ya kuwafunga bila huruma Mtakuja Beach
5-1 katika mchezo wa fainali wa mashindano hayo ya vijana chini ya umri
wa miaka 17. Mchezo huo ulifanyika kwenye kiwanja cha shule ya Msingi
Mwananyamala jijini Dar es Salaam leo Juni 25 ,2013.
Mabingwa
hao wapya wa ARS ngazi ya mkoa walianza michuano hiyo kwa kishindo
walipoitandika Sifa United 3-1 katika mchezo wa ufunguzi uliopigwa
katika uwanjwa huo huo Jumapili. Katika mchezo wa leo, Makumbusho
wamepata magoli kupitia kwa Premji Stephano (dk 12), Ally Amin (dk 35),
Rashid Ngone (dk 38 na 71) na Wllie Kalolo (dk 53) wakati Mtakuja
walipata goli la kufutia machozi dakika ya 78 kwa njia ya penati
iliyopigwa na Steven Munyu.
Jijini Mbeya, timu
ya Mbasco ilitoshana nguvu na timu ya Mbosa Jumatatu Juni 24 baada ya
kutoka sare ya 3-3 katika mchezo wa vuta nikuvute wa Airtel Rising
Stars. Mbasco walipata magoli yao kupitia kwa Jasco Mwaibabe (dk 20 na
50) na Joel Kasimila dakika ya 68. Mchezo huo ulifanyika kwenye kiwanja
cha Magereza Mbeya.
Kwa
upande wao, Mbosa walipata magoli yao kupitia kwa Michael Mwashilanga
(dk 5), Richard Kalinga (dk 49) na Enock Chikaonga (dk 9).
Mjini Morogoro;
timu ya Moro kids iliishinda Anglikana 3-0 katika mchezo mwingine wa
Airtel Rising Stars ngazi ya mkoa uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya
seconday ya Morogoro. Magoli ya Moro kids yaliwekwa kimiani na Abdul
Rashid, Robert Nashon na Evans Nashon. Robert na Evans ni mapacha.
Katika
mkoa wa kisoka wa Ilalan, Msimamo Youth Academy walipata ushiindi
mwembamba wa 1-0 dhidi ya Buguruni Youth Center katika mchezo mgumu
iliofanyika kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam.
Goli hilo la ushindi lilifungwa dakika za majeruhi na nahodha wa timu
hiyo Rajab Mohamed katika dakika ya 89
Mkoa
wa kisoka waTemeke ulitarajiwa kuanza mechi zake za Airtel Rising Stars
ngazi ya mkoa jana (leo) katika uwanja wa Twalipo na mkoa wa Mwanza
vile vile ulitarajia kuanza mechi zake kwenye uwanja mkongwe wa
Nyamagana jana (leo).
Programu
hii ya Airtel Rising Stars ni ya Afrika nzima likiwa na lengo la
kuendeleza na kukuza mpira wa miguu katika bara la Afrika kwa vijana
wanaochipukia waweze kupata nafasi ya kuendeleza vipaji vyao.
Fainali
za ARS Taifa vile vile zitatumika kuchagua timu bora za wavulana na
wasichana ambao wataiwakilishaTanzania katika mashindano ya kimataifa
ambapo nchi mwenyeji wa michuano hiyo itatangazwa mwezi ujao. Wachazeaji
wengine watachaguliwa kwenda kwenye kliniki itakayoendeshwa na makocha
kutoka klabu maarufu duniani ya Manchester United
0 comments:
Post a Comment