Na Baraka Mpenja wa
Mshambuliaji
nyota wa maafande wa Tanzania Prisons, Elius Maguli ametimkia zake kwa
wapigwa kwata wa Ruvu Shooting wa mkoani Pwani baada ya kukubali kumwaga
wino na kusaini kuitumika timu hiyo kwa miaka mwili.
Afisa habari wa Ruvu Shooting Masau Bwire ameimabia MATUKIO DUNIANI
Kuwa Maguli ni moja kati ya washambuliaji hatari kwa sasa kwani msimu
uliopita alipachika mabao 5 kimiani na kuisaidia Prisons kusalia ligi
kuu, hivyo ana uwezo mkubwa wa kuipeleka mbele klabu hiyo inaoyonolewa
na kocha Charles Boniface Mkwasa “Master”.
“Maguli
ni bunduki yetu sasa, tunafanya usajili makini, kocha wetu alipendekeze
wasajiliwe wachezaji nane, tunaendelea kusaka vipaji vya hali ya juu,
hatutaki majina makubwa bali tunataka wachezaji wenye uwezo wa
kutusaidia msimu ujao”. Alisema Masau.
Masau
alitamba kuwa timu nyingi zinasajili majina makubwa, wakisikia
walicheza Simba na Yanga wanaona wanafaa, kumbe ni ugonjwa tu, hivyo wao
wanasaka vipaji vipya kwa sasa.
Afisa
habari huyo aliongeza kuwa wanataka kufanya usajili mkubwa ili msimu
ujao waweze kufuta ufalme wa klabu za Simba na Yanga katika harakati za
kuwania ubingwa.
“Kila
mwaka Simba na Yanga, wanapokezana ubingwa kama mbio za vijiti, sisi
Shooting msimu ujao tunakuwa watu wa kwanza kupindua ufalme wa timu hizi
mbili. Inawezekana sana na ndio maana tunasajili vifaa vipya”. Alisema
Masau.
Mbali
na kuweka wazi usajili huo, afisa habari huyo hakusita kujibu tetesi
zilizoenea kwamba wekundu wa Msimbazi Simba wamemsajili mshambuliaji
nyota wa klabu hiyo Hassan Dilunga kwa mkataba wa miaka miwili.
Masau
alisema viongozi wa klabu hiyo hawana taarifa yoyote kuhusu usajili huo
na Simba hawajazungumza lolote mpaka sasa, lakini wanawasubiri kukaa
meza moja kwani bado Dilunga ana mkataba wa mwaka mmoja na maafande hao.
“Dilunga
ni mchezaji wetu, bado tuna mkataba naye, sidhani kama itakuwa busara
kwa Simba kumsajili bila kuongea na viongozi wa Shooting, sisi
tunawasubiri ili kujibu tetesi hizo”. Alisema Masau.
0 comments:
Post a Comment