Na Baraka Mpenja kwa msaada Sportsmail.com
Mabingwa
wa soka nchini England, mashetani wekundu, Manchester United wapo
mbioni kuinasa saini ya kiungo fundi wa klabu ya FC Barcelona, wazee wa
Katalunya, “Maestro” Thiago Alcantara kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 17.
United
wamewaingilia wapinzani wao Man City kwa kukubaliana na Thiago pamoja
na baba yake Mazinho ili wamlipe nyota huyo pauni milioni 5 kwa mwaka,
ikumbukwe hata City walishatangaza kumtaka mtaalamu huyo mwenye umri wa
miaka 22.
Kwa
mujibu wa vyanzo vya habari, dili hilo halijakamilika kwa sasa, lakini
leo hii taarifa inaweza kutolewa kutoka klabuni hapo, huku mazungumzo
zaidi yakitarajiwa kufanyika wikiendi ya wiki hii.
Nyota
ya Thiago inawaka vilivyo katika sokamla Hispania, lakini amejiongezea
thamani zaidi baada ya kuisadia timu yake ya taifa ya vijana kutwaa
ubingwa wa mataifa ya Ulaya mapema wiki hii huku akipiga mabao matatu
peke yake ” hat-trick” dhidi ya Italia.
Mbali ya kuwa na kiwango cha juu kinda huyo hana namba ya kudumu katika
dimba la Nou Camo licha ya klabu hiyo kuonekana kumtegemea zaidi siku
za usoni ili kuendeleza ufalme wao wa soka la dunia.
Anatua
Old Traford: Thiago Alcantara ataweza kuimarisha safu ya kiungo ya
Manchester United baada ya mkongwe mwenye kipaji cha ajabu Paul Scholes
kutandika daluga zake kucheza kandanda
Kipaji cha kutisha: Barcelona bado wanaamini kuwa nyota wao Thiago atakuwa mchezaji muhimu wa kikosi chao miaka ijayo
Mstaafu: Paul Scholes ameacha majanga katika safu ya kiungo ya Man United, sasa wanahitaji mtu wa kurithi mikoba yake
0 comments:
Post a Comment