Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam
IMEWEKWA JUNI 24, SAA 11:56 ASUBUHI
Maandalizi
ya mashindano ya ngumi za ridhaa kwa majiji ya Afrika Mashariki
yatakayofanyika jijini Mwanza mwezi ujao yanaendelea vizuri huku majiji
mbalimbali yakijiandaa kushindana na si kushiriki.
Katibu mkuu wa shirikisho la ngumi za ridhaa Tanzania , BFT, Kiongozi Makore Mashaga amezungumza na mtandao wa kazi wa FULLSHANGWE
na kuhabarisha kuwa Mwanza ndio waandaaji wakubwa wa mashindano ya
mwaka huu, lakini taarifa alizopokea ofisini kwake ni kuwa maandalizi
yanakwenda vizuri huku majiji ya nje yakithibitisha ushiriki wao.
“Majiji
ya Kampala, Nairobi, na Bujumbula tayari yamethibitsha kushiriki,
wakati kwa Tanzania majiji ya Mwanza ambao ndio wenyeji, Tanga, Dar es
salaam, pia Manispaa ya Temeke, pamoja na Mbeya, Arusha yakiendelea na
maandalizi yao”. Alisema Mashaga.
Mashaga
alisema mwaka huu mipango yao ni kuhakikisha majiji ya Tanzania
yanaonesha umwamba mkubwa mbele ya wageni, na kwa kutambua hilo
wameagiza majiji yote kujipanga vilivyo ili kukamilisha nia hiyo ya BFT.
Katibu
huyo ameongeza kuwa katika mashindano ya mwaka huu wameamua kuongeza
timu za vyombo vya ulinzi na usalama, kwa maana ya timu za Jeshi la
wananchi Tanzania JWTZ, JKT na Magereza kwa kuzingatia umuhimu wao
katika mchezo wa ngumi.
Pia
wametambua ushiriki wao katika mchezo wa ngumi ambapo wachezaji wengi
wa timu ya taifa ya ngumi za ridhaa hutokea katika timu hizo.
“Kutokana
na mchango wao katika mchezo wa ngumi hapa nchini, tumeamua
kuwashirikisha nao, kwa hiyo mashindano ya mwaka huu yatakuwa mazuri
sana”. Alisema Mashaga.
Mashindano
ya mwaka huu yataambatana na uchaguzi mkuu wa BFT ambao utafanyika
Julai 7 mwaka huu jijini Mwanza, na tayari zoezi la uchukuaji wa fomu za
kuwania nafasi mbalimbali linaendelea chini ya baraza la michezo la
taifa BMT ambao ndio wasimamizi wakuu.
0 comments:
Post a Comment