Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Nahodha
wa zamani wa washika bunduki wa jiji la London, klabu ya Asernal,
Lejendari Tony Adams amesikitishwa na kitendo cha uongozi wa klabu hiyo
kumnyima nafasi ya kuingia katika bodi ya klabu hiyo kwa lengo la
kuifufua timu .
Adams
mwenye umri wa miaka 46 kwa sasa alimuandikia barua mwenyekiti wa
Arsenal, Peter Hill-Wood baada ya uongozi wa klabu hiyo inayokabiliwa na
ukame wa makombe kutangaza kuwa wanahitaji damu changa kuongoza timu.
Adams
aliyekuwa nahodha mkubwa katika historia ya Arsenal aliomba kujiunga na
klabu hiyo kwa kuwa mjumbe wa bodi bila malipo yoyote, lakini
hakujibiwa maombi yake, na baadaye akasikia mmiliki wa klabu hiyo, raia
wa Marekani Stan Kroenke amemteua Chips Keswick mwenye umri wa miaka 73 kuwa mwenyekiti wa klabu.
Adam ameliambia gazeti la Sun kuwa hataki fedha, lakini anataka kutumia nafasi hiyo kuirudisha klabu katika ulimwengu wa makombe
“Chips
ni mtu mkubwa, lakini sio chagua sahihi. Ana miaka 73 kwa sasa, umri
umeenda sana na klabu inahitaji kijana wa kuisaidia”. Alisema Adams.
Bure kabisa: Lejendari wa Arsenal Tony Adams amekatishwa tamaa kuisaidia klabu yake ya zamani
Enzi hizo Adam akiwa na washika bunduki wa London akiwa nahodha
Kazi imeanza: Mwenyekiti mpya wa Arsenal Sir Chips Keswick
Hofu kubwa: Adams amesema Arsenal hawana maandalizi yoyote endapo Arsene Wenger ataamua kutimka zake.
Amesena ni muda muafaka kwa Arsenal kutwaa taji hata la kombe la FA au kombe la Ligi, lakini haoni kama inawezekana kwa sasa.
0 comments:
Post a Comment