Thursday, June 6, 2013


Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Lejendari wa soka raia wa Brazil, Pele, anaamini kuwa kurejea kwa kocha mwenye maneno mengi, The spesho Jose Mourinho katika klabu yake ya zamani ya Chelsea ya jijini London ni chagua sahihi kwa klabu hiyo.
Mashabiki wengi wa klabu ya Chelsea wanaamini kuwa kurejea kwa Mourinho darajani, mataji ya ligi kuu yatarejea tena klabuni hapo kama miaka ya 2005 na 2006.
Ingawa Pele anakubaki maamuzi ya Roman Abramovich kumrejesha Mourinho, lakini ameonya kuwa kurejea kwa kocha huyo sio sababu ya kutegemea mafanikio makubwa.
Pele mwenye umri wa miaka 72, ameimbia televisheni ya CNN  kuwa kurejea kwa Mourinho katika klabu ya Chelsea ni jambo zuri kwani ni kocha bora.
“Ni kocha mwenye kipaji kikubwa na mkweli. Najua sana. Lakini soka lina maajabu yake. Ana bahati sana katika kazi yake, wakati mwingine kizuri huwa hakifanikiwi”. Alisema Pele.
Back in town: Pele believes Chelsea have made the right move to bring Mourinho back to Stamford Bridge 
Amerudi mjini: Pele amesema Chelsea imefanya maamuzi sahihi kumrejesha Mourinho darajani
The New Pele: Barcelona's Neymar, 21, has long been hyped up after his impressive performances for Santos
Pele Mpya: Nyota wa Barcelona  Neymar, mwenye umri wa miaka 21, amewavutiwa wengi na kutajwa kuwa Pele mpya wa Brazil
Wiki hii pia habari kubwa wiki hii ni  Neymar kutimka katika klabu ya Santos ya Brazil, klabu ambayo Pele alicheza na kuifungia mabao 589 katika michezo 605 kuanzia mwaka 1956-1974.
Neymar ameifungia Santos mabao 54 katika mechi 103 na sasa anatajwa kuwa Pele mpya wa Brazil, lakini kwa upnde wake Pele anakataa kumfananisha na kinda huyo wa dunia.
Playing it cool: Pele has played down the comparison but agrees that Neymar is one of Brazil's best players 
Pele amekataa kulinganishwa na bwana mdogo Neymar, lakini amekiri kuwa kijana huyo ni moja kati ya wachezaji bora zaidi kuwahi kutokea nchini Brazil
Pele alisema ” Neymar kuwa kama Pele mpya ni jambo gumu sana kwa sababu mama yangu na baba yangu walishamaliza kazi ya kuzaa”.
Pele aliendelea kueleza kuwa hakuna shaka kabisa kuwa Neymar ni moja kati ya vipaji vikubwa nchini Brazil.
“Kiukweli Brazil vipaji vingi vimewahi kutokea kama Zico, Tostao, Rivelino, Pele, Ronaldinho, lakini kwa miaka miwili iliyopita, Neymar ana kipaji kikubwa zaidi”. Alisema Pele.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video