Kocha
mkuu wa Twiga Stars, Rogasian Kaijage akitoa somo kwa makocha
wanashiriki kozi ya ukocha ngazi ya pili ndani ya darasa kwenye Ukumbi
wa Harbours Club, Kurasini.
Kocha mkuu wa Twiga Stars akitoa somo kwa makocha wa kozi ya ngazi ya pili kwa vitendo
KOZI
ya makocha wa ngazi ya pili (Intermediate) inayosimamiwa na Chama cha
Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), inatarajiwa kufungwa
Jumanne ijayo baada ya kudumu kwa wiki nne.
Kozi
hiyo ilianza Juni 3 mwaka huu kwenye Ukumbi wa Harbours Club, uliopo
Kurasini chini ya Mkufunzi Rogasin Kaijage, ambaye ni Kocha wa timu ya
Taifa ya Wanawake ‘Twiga Stars’ ambapo makocha mbalimbali pamoja na
wachezaji wa zamani wamejitokeza kushiriki.
Ofisa
Habari wa DRFA, Mohamed Mharizo alisema kozi hiyo imekuwa na mafanikio
na wanatarajia makocha walioshiriki katika kozi hiyo watakuwa na mchango
mkubwa katika kuendeleza mpira wa miguu katika mkoa wa Dar es Salaan na
Taifa kwa ujumla.
“Hadi
sasa tunashukuru kuona tunafanikisha kozi hii ambayo wengi wameitikia
wito, mwisho wa kozi hii ndio mwanzo wa kozi nyingine.
“Lakini
haya ya kozi ya makocha ni moja ya majukumu ya Kamati ya Ufundi ya DRFA
yaliyoainishwa katika Katiba, hivyo hili ni moja ya shabaha yetu na
mengine mengi mazuri yanafuata,” alisema Mharizo.
Kozi
hiyo ni ya kwanza kuendeshwa na DRFA tangu kuingia madarakani kwa
uongozi mpya wa chama hicho Desemba 12, chini ya Mwenyekiti wake Almas
Kassongo.
0 comments:
Post a Comment