Imewekwa June 24, 2013, saa 12: 01 mchana
Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
KOCHA wa Norwich, Chris Hughton anapambana kuipiga bao Everton katika kuwania saini ya mshambuliaji wa Wigan, Arouna Kone
Mkataba wa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast ua thamani ya Pauni Milioni 5. Msimu uliopita amefunga mabao 13 na kuisaidia Wigan kutwaa Kombe la FA. Hull, Liverpool na Crystal Palace zote zinamtaka pia.
Uwezekana
wa kuungana tena: Wakiwa wametwaa Kombe la FA pamoja Wigan msimu
uliopita, Arouna Kone (kushoto) anaweza kuungana tena na kocha mpya wa
Everton, Roberto Martinez (kulia).
Jumapili,
Kone alizipigia kengele klabu kubwa baada ya kusema hayuko tayari
kucheza Daraja la Kwanza, kufuatia Wigan kushuka daraja.
Akizungumza
na The Sun, nyota huyo wa zamani wa PSV Eindhoven alisema: “Wakati wote
una malengo kama mchezaji, na siko tayari kucheza ligi ya pili England.
“Wigan
imeshuka, ambayo ni aibu kubwa. Ni juu yao kuweka mambo sawa juu ya
mipango yangu. Mimi ni wa kucheza moja ya klabu bora England, na
natumai nitapata nafasi.
0 comments:
Post a Comment