Baraka Mpenja
Mtunzi
wa kitabu cha “SOKA LA TANZANIA”, katibu mkuu wa zamani wa TFF,
Fredrick Mwakalebela ameendelea kuwashukuru watanzania kwa kumuunga
mkono kwa kuendelea kununua nakala za kitabu hicho kwa thamani ya
shilingi elfu kumi tu (10,000/=).
Mwakalebela ameimbia MATUKIO DUNIANI
kuwa tangu azindue rasmi kuuza kitabu hicho katika mechi ya watani wa
jadi, Simba na Yanga mnamo mei 18 mwaka huu, watanzania wanaonesha
muitikio mkubwa sana, hivyo anawashukuru sana kwa kitendo hicho.
“Kwa
kweli nitakuwa mnyimi wa fadhila kama sitawashukuru watanzania kwa moyo
walioonesha, wananunua kitabu cha SOKA LA TANZANIA na kunipa matumaini
ya kuwafikia watu wengi wanaopenda mpira wa Tanzania”. Alisema
Mwakalebela.
Katibu
huyo wa zamani wa TFF, aliongeza kuwa kwa sasa wameshakamilisha mipingo
yote ya kusambaza kopi za kitabu hicho mikoani, hivyo watanzania
waishio maeneo hayo wakae mkao wa kula kwani muda si mrefu kitabu
kitawasili maduka mbalimbali ya vitabu.
“Wiki
ijayo kila kitu kitaenda sawa, nakala kutosha zimeshaandaliwa kwa ajili
ya watu wa mikoani, kikubwa watu wa huko wajiandae, hakika kina mambo
mengi ndani yake na mtu hatapoteza hela yake”. Alisema Mwakalebela.
Akizungumzia
kilichaoandikwa ndani ya kitabu hicho, Mwakalebela alisema kuna mambo
mengi sana, lakini kubwa ni maendeleo ya soka la Tanzania kwa kuangalia
timu za vijana, michauno ya vijana, timu ya taifa, mchango wa serikali
ya DKT. Jakaya Kikwete kuendeleza soka la Tanzania, Historia na maisha
ya Kocha Marcio Maximo kutoka Brazil, Historia ya timu ya taifa,
kumbukumbu ya magoli ya stars na vikosi vyake vya nyuma pamoja na mambo
mengine mengi yahusuyo soka la Tanzania.
Kitabu
cha SOKA LA TANZANIA kilichoandikwa na Mwakalebela ni cha kwanza
kutokea nchini Tanzania, hivyo ni nafasi ya Mtanzania yeyeto Yule kupata
nakala ili kujifunza mambo mengi ya soka la Tanzania wakiwemo makocha,
waandishi wa habari za michezo pamoja na wachezaji kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment