Na Baraka Mpenja
Kocha
wa wekundu wa Msimbazi Simba mzee Abdallah Kibadeni “King Mputa”
amewataka mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kuwa wavumilivu kwa
wakati huu ambao wamekubali timu isukwe upya kwa ajili ya michuano ijayo
ya ligi kuu Tanzania bara.
Kibadeni
ameyasema hayo katika mazoezi ya mwisho ya kubaini wachezaji wapya kwa
ajili ya kuwasajili kwa ajili ya kikosi cha vijana chini ya umri wa
miaka 20 pamoja na wachezaji kutoka sehemu mbalimbali kufanya majaribio
yao kujaribu bahati ya kusajiliwa na Simba msimu ujao.
Wachezaji
kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi wapo katika mazoezi
makali chini ya benchi la klabu ya simba linaloongozwa na Kibaden pamoja
na Jamhuri Kihwelu, Amri Said na Selemani Matola.
“Kama
wamekubali timu ijenge upya ili kurudisha heshima iliyopotea baada ya
kufanya vibaya msimu uliopita na kupokonywa ubingwa na watani zetu wa
jadi Yanga, kinachotakiwa kwao ni utulivu mkubwa sana na kutokuwa na
haraka kwani timu haijengwi kwa siku moja”. Alisema Kibadeni.
Kocha
huyo ambaye msimu uliopita alikuwa na kikosi cha wakata miwa wa
Kaitaba, Kagera Sugar aliongeza kuwa kwa sasa anaandaa kikosi cha
kushiriki michuano ya kombe la Kagame litakalofanyika mwezi huu nchini
Sudan.
Kibadeni
aliyewahi kuichezea Simba kwa mafanikio miaka ya sabini na kuifundisha
kwa mafanikio makubwa alisisitiza kuwa michuano ya Kagame itakuwa kipimo
tosha kwa kikosi chake kwani atawapima wachezaji wake na kama kutakuwa
na mapungufu basi ataongeza nyota wengine.
“Kombe
hili nitapima makali ya kikosi changu, nikigundua kuwa kina matatizo
basi nitaaangalia namna ya kutafuta wachezaji wengine kwani usajili
utakuwa bado haujaisha”. Alisema Kibadeni.
Tayari
simba ambayo ilimaliza ligi katika nafasi ya tatu imeshasajili baadhi
ya wachezaji ambao ni Zahoro Pazi, Issa Rashid, Ibrahim Twaha almaarufu
kwa jina la Messi, Andrew Ntara pamoja na Moses Oloya.
Lakini
imeondokewa na winga machachari anayeichezea Taifa Stars Mrisho Ngasa
aliyejiunga na Yanga lakini hilo halimtetemeshi Kocha msaidizi wa Simba,
bwana Kihwelu.
“Kuondoka
wa Ngassa sio pengo kwetu, mpira ni kazi yake, mimi nadhani Simba ni
klabu kubwa ambayo haiwezi kumbani mchezaji, muache akacheze huko,
lakini sisi tuko sawa, hakuna tatizo lolote”. Alisema Kiwhelu.
0 comments:
Post a Comment