Sunday, June 16, 2013

Kim Paulsena amesema vijana wake wana morali kubwa sana kukabiliana na timu bora zaidi barani Afrika, Ivory Coast na leo lazima Taifa stars ipate ushindi wa nyumbani 120
Na Baraka Mpenja
Muda mfupi kabla ya kushuhudia kipute cha kukata na mundu baina ya timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa stars dhidi ya Tembo kutoka pwani ya magharibi mwa Afrika, Ivory Coast, mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia mwakani nchini Brazil, Kocha wa Taifa Stars, Kim Paulsen amewahakikishia Watnzania wote kuibuka na ushindi katika mechi hiyo ngumu ya kundi C.
Akiongea na mtandao huu, Kim amesema kikosi chake kina morali kubwa kuvaana na Ivory Coast ambao ni bora zaidi kwa kucheza soka barani Afrika.
“Ivory Coast ni timu ya kwanza kwa ubora barani Afrika, wachezaji wangu huwa wanafurahi sana kucheza na timu bora. Imani yangu ni kwamba, vijana watacheza soka zuri na kuwabamiza wapinzani wetu hao”. Alisema kim.
Kocha huyo amesema kukosekana kwa wachezaji wake wawili wa kikosi cha kwanza, Mrisho Ngassa na Agrey Moriss ambao wanatumikia adhabu ya kadi, kwamaana ya kadi nyekundu kwa Moriss ambapo mlinzi huyo alipata nchini Morocco huku Ngassa akiwa na kadi mbili za njano, hakutaathiri kikosi chake kwani kuna wachezaji wengi wenye uwezo wa kufanya vizuri.
“Sio wakati wa kuzungumzia nani atakosekana, kikosi changu kina wachezaji zaidi ya Ishirini, leo hii Canavaro ataziba nafasi ya Moriss, lakini kwa suala la Ngassa bado nina wachezaji wengi wa kuchukua nafasi yake, ingawa hali hii pia imeniwazisha sana”. Alisema Kim.
Kwa upande wa Nahodha wa Stars, Juma  Kaseja ameimbia MATUKIO DUNIANI kuwa wanawaheshimu sana wapinzani wao kwa maana ya ubora wao, lakini hawaogopi kitu kwani wanaweza kufungika katika mchezo huo.
“Ivory Coast wametutangulia kimchezo, lakini haina maana tunawaogopa, tuko sawa, tumefanya maandalizi mazuri na leo hii lazima tuibuke na ushindi ili kuwapa raha mashabiki wetu walioanza kuingia uwanjani”. Alisema Kaseja.
Kikubwa Kaseja amewaomba Watanzania kuwaombea dua njema wachezaji wao ili leo waibuke na ushindi muhimu mbele ya miamba hiyo ya Afrika.
Naye Nadir Haroub Canavaro amefurahishwa sana na kitendo cha kupata namba katika kikosi cha kwanza cha Taifa stars katika mechi ya leo.
“Ni mechi ngumu sana, mimi huwa nafurahi sana kucheza mechi ngumu kwani inanijengea historia nzuri, hivyo nimefurahi sana kuanza leo na lazima nicheze kufa na kupona kuisaidia timu yangu”. Alisema Canavaro.
Naye Frank Domayo amesema kuwa mchezo wa leo wamejiandaa kupata ushindi ingawa wanatambua ubora wa wapinzani wao.
“Binafasi najisikia furaha sana kucheza kikosi cha kwanza katika mchezo wa leo, nimekuwa nikiimarika sana katika michezo mikubwa, nafikiri leo pia nitatumia nafasi yangu kuisaidia Stars”. Alisema Domayo.
Kwa upande wa mchezaji nguli wa Ivory Coast,  Solomon Kalou ameimbai MATUKIO DUNIANI  Kuwa mchezo wa leo ni mgumu sana, lakini Taifa stars bado ni timu ndogo hivyo watafungwa tu.
“Walicheza vizuri nyumbani na kutupa changamoto, lakini nafikiri bado ni wachanga sana, tutawafunga ingawa kila timu ina nafasi ya kushinda”. Alisema Kalou.
Mchezo wa stars unatarajiwa kuanza majira ya saa tisa alasiri katika dimba la taifa jijini Dar es salaama na tayari joto la mechi hiyo limeshapanda vya kutosha huku watu wakiingia uwanjani.
Mchezo wa kwanza Stars walifunga mabao 2-0 jijini Abijan nchini Ivory cOsta mwaka jana.
Kila la kheri stars katika mchezo wa leo.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video