kikosi cha Simba |
Na Baraka Mpenja
Benchi la ufundi la Wekundu wa Msimbazi Simba “Taifa Kubwa”
limepata jeuri kubwa baada ya kusuka wachezaji wengi makinda na kusema kuwa
mwenye nidhamu mbovu kuanzia nje ya uwanja na ndani ya uwanja, kamwe hapati
nafasi katika kikosi cha klabu hiyo msimu ujao wa ligi kuu Tanzania bara.
Kocha msadizi wa klabu hiyo aliyebarikiwa kuwa na maneno
mengi, Jamhuri Kiwhelo “Julio” alisema kuwa kutokana na kusuka kikosi bora cha
vijana, wanahitaji kuona timu hiyo inatawaliwa na nidhamu kubwa tofauti na
msimu uliopita ambao Simba alikuwa na tatizo la wachezaji wake kukosa nidhamu
na kutemwa na aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Mfaransa Patrick Liewig.
Miongoni mwa wachezaji walioangukia katika rungu la kutemwa kutokana
na tuhuma za utovu wa nidhamu ni pamoja na Haruna Moshi “Boban”, Ramadhan Chombo
“Redondo”, Ferlix Sunzu, Mwinyi Kazimoto Mwitula, Abdallah Juma, Amir Maftah,
Juma Nyoso na wengineo, na sasa baadhi ya nyota hao wengi wametemwa katika
usajili.
“Safari hii hatutaweza kumvumilia mchezaji mwenye nidhamu
mbovu kwani atarudisha nyuma malengo yetu ya kuwa na kikosi bora kuliko timu
zote Tanzania na Afrika kwa ujumla”. Alisema Julio.
Julio aliongeza kuwa benchi la ufundi chini ya kocha mkongwe
Abdallah Kibaden “King Mputa” kamwe halitafumbia macho suala la utovu wa
nidhamu ili kukamilisha malengo yao ya kurejesha taji Msimbazi baada ya msimu
uliopita kupokonywa na watani wao wa jadi Yanga na wao kuishia nafasi ya tatu
katika msimamo.
“Simba hii lazima watu wataipenda tu, nidhamu ndio msingi
katika kikosi chetu, nasisitiza tena kama mchezaji atakuwa mtovu wa nidhamu,
bila kujali jina lake, katu hapati nafasi katika kikosi chetu”. Alisema Julio.
Kocha huyo ambaye alifanya kazi na Liewig msimu uliopita,
aliongeza kuwa mashabiki wa klabu hiyo wanatakiwa kuwa karibu na timu ili
kuwapa moyo vijana wao na kufika mbali zaidi.
“Kwanza tumshkuru Mungu hapa tulipofika, wakati
tumeanza mpango wa kuijenga Simba ya vijana, watu walijua tunatania, lakini
tuko vizuri na sasa tunasuka kikosi
0 comments:
Post a Comment