Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Historia: Fomu ya kikosi cha kwanza cha Sir Alex Ferguson kuiongoza Manchester United imepigwa mnada.
Kikosi hicho alichoandika
Sir Alex Ferguson akiiongoza timu hiyo kwa mara ya kwanza imeuzwa
kwenye mnada kwa Pauni 19,500, mara sita ya bei iliyotakiwa.
Kwa
Mara ya kwanza, United inajiandaa kwa maisha bila Alex Ferguson tangu
mwaka 1986, huku David Moyes akijiandaa kurithi mikoba yake kwa kuanza
kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya England.
Lakini
fomu hiyo ya kikosi, iliyoandikwa kwa mkoko wa Ferguson na kusainiwa
naye katika mchezo ambao walichapwa 2-0 na Oxford United, Novemba 8,
mwaka 1986 unaleta kumbukumbu ya namna gwiji huyo alivyoanza kazi.
Iliuzwa mjini Devizes, Wiltshire, kwa Muingereza ambaye ni shabiki wa Oxford.
Ilipangiwa kuuzwa kwa Pauni 3,000 lakini mwishowe ikafikia bei hiyo baada ya mchuano wa China na Marekani.
Wachezaji
maarufu na nyota kama Paul McGrath na Arthur Albiston wamo kwenye
kikosi hicho, sambamba na wenmgine wanaokumbukwa kama kipa Chris Turner
na Graeme Hogg.
Wakati
huo hakukuwa na mchezaji hata mmoja kati ya wale maarufu aliowasajili
wakiwa makinda kama Peter Schmeichel au Ryan Giggs Old Trafford.
Pia kuna kikosi cha mwisho cha Mscotland huyo ambacho kilitoka sare ya 5-5 ugenini na West Brom.
Pia
kimeandikwa kwa mkono wake Ferguson – kikionyesha nyota kadhaa wa
kimataifa kama Robin Van Persie na Nahodha Michael Carrick.
Wakongwe
wa United, Ryan Giggs na Paul Scholes, ambao pia walicheza kwa mara ya
mwisho, walikuwemo katika orodha ya wachezaji wa akiba.
Pamoja
na hayo, msaidizi wa David De Gea, Anders Lindegaard, jina lake
lilikosewa katika karatasi hiyo kwa herufi ‘r’ kutumika katika jina
lake.
Mechi ya kwanza: Alex Ferguson (kulia) akiingalia timu yake mpya ya Manchester United katika Uwanja wa Oxford United, uitwao Manor Ground.
0 comments:
Post a Comment