Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Katika
harakati zake za kuimarisha kikosi cha washika bunduki wa London, Kocha
wa klabu hiyo, Mfaransa Arsene Wenger amesema timu hiyo inaendelea na
mazungumzo ya kina na nyota wa Real Madrid ya Hispania Gonzalo Higuain
ili kuinasa saini ya mshambuliaji huyo kwa ada ya uhamisho wa pauni
milioni 20.
The
Gunner hawana imani ya kumpata Stevan Jovetic baada ya Chelsea kuonesha
nia ya kumsajili kwa kitita cha kutosha, sasa hesabu zao ni kwa Higuain
ambaye pia anawaniwa na miamba ya soka la Italia, Juventus.
Wakati
Wenger akihaha katika usajili, bado ndoto yake kubwa ni kumpata nyota
wa mashetani wekundu, Machester United, Wayne Roooney ambapo amekubali
kuvunja benki ili kumnasa nyota huyo aliyeonesha nia ya kutaka kuihama
United.
Wakati
Mfaransa huyo akitanga na ya kumtaka Higuain, nyota huyo amekiri
kupenda kuhamia Emirates endapo watamlipa kile anachokihitaji.
Higuain
mwenye umri wa miaka 25 kwa sasa, akiwa Real Madrid anavuta mkwanja wa
pauni laki mbili na elfu thelathini kwa wiki, pesa ambayo ipo chini ya
uwezo wa Arsenal.
London inamuita: Gonzalo Higuain (katikati) yupo katika rada za bosi wa Arsenal, mzee Arsene Wenger
Huyu ndio kila kitu: Stevan Jovetic (kuahoto) anawindwa na timu nyingi za ligi kuu nchini Uingereza
Wakati
huo huo Marseille wanamtaka mshambuliaji wa Arsenal, Gervinho kwa
mkopo. Huku Barcelona wakimhitaji beki wa Arsenal Thomas Vermaelen.
0 comments:
Post a Comment