John
Bocco leo hii ataongoza safu ya ushambuliaji ya Taifa stars, akitumia
nafasi hii atajijengea mazingira ya kuanza kule Morroco, manake jembe
Samata na Ulimwengu watakuwepo
Samata
na Ulimwengu hawapo katika mechi ya leo dhidi ya Sudan nchini Ethiopia,
jembe kiemba yupo kama kawaida kusimamia mpango wa dimba la kati na
vijana kama Domayo
Na Baraka Mpenja
TIMU
ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars chini ya kocha Kim Paulsen ,
leo inatarajiwa kushuka dimbani kwenye Uwanja wa Addis Ababa nchini
Ethiopia kupepetana na Sudan ‘Mamba wa Mto Nile’ katika mchezo wa
kirafiki ulio kwenye kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Stars
leo hii itaongozwa na mshambuliaji wa Azam FC, John Raphael Bocco
“Abebayor” kufuatia kukosekana kwa nyota Mbwana Ally Samata na Thomas
Emmanuel Ulimwengu ambao hawajajiunga na timu hiyo mpaka sasa kutokana
na kuwa na majukumu ya kutumikia kibarua chao TP Mazembe katika Kombe la
Shirikisho Afrika.
Bila
shaka John Raphael ‘Bocco’ atasimama badala ya Samatta na kipindi cha
pili kocha Kim Paulsen anaweza akayahamishia majukumu ya Ulimwengu kwa
Zahor Pazi au Simon Msuva, itategemea na aina ya mchezo na wapinzani.
Taifa
Stars ambayo iko Addis Ababa tangu Jumatatu (Mei 27 mwaka huu) imeweka
kambi katika hoteli ya Hilton kujiandaa na mchezo wa Kundi C dhidi ya
Morocco Juni 8 mjini Marakech kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe
la Dunia mwakani nchini Brazil.
Lakini
kwa asilimia kikubwa kikosi cha Stars kinatarajiwa kuwa kile kile
kilichocheza na Morocco katika mchezo wake wa mwisho Machi 22 mjini Dar
es Salaam; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Shomary Kapombe, Kevin Yondan,
Aggrey Morris, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Mrisho Ngassa, Athumani Iddi,
Frank Domayo, John Bocco na Amri Kiemba.
Kwenye benchi wanaweza kuwapo Ally Mustafa ‘Barthez’, Mwinyi Kazimoto, Mudathir Yahya, Simon Msuva, Zahor Pazi, Mwadini Ally, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Khamis Mcha, Vicent Barnabas na Haroun Chanongo.
Kwenye benchi wanaweza kuwapo Ally Mustafa ‘Barthez’, Mwinyi Kazimoto, Mudathir Yahya, Simon Msuva, Zahor Pazi, Mwadini Ally, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Khamis Mcha, Vicent Barnabas na Haroun Chanongo.
Balozi
wa Tanzania nchini Ethiopia, Joram Biswaro anatarajiwa kuwaongoza
Watanzania wachache waliopo nchini humo kwenda kuishangilia Taifa Stars.
Balozi
Biswaro ameikaribisha Taifa Stars ubalozini Addis Ababa mara baada ya
mechi dhidi ya Sudan ambapo itakutana na baadhi ya Watanzania wanaoishi
Ethiopia kabla ya kuondoka alfajiri kwenda Marrakech, Morocco kwa
kupitia Cairo, Misri.
Kocha
Kim Poulsen amesema kikosi chake kinaendelea na mazoezi vizuri na
kitaimarika zaidi baada ya Samatta na Ulimwengu kujiunga na wenzao Juni 3
mwaka huu mjini Marrakech.
0 comments:
Post a Comment