HALMASHAURI
ya Wilaya ya Ilala, imesema operesheni ya kuwaondoa wafanya biashara
wadogo wadogo kwenye maeneo ambayo si rasmiitakuwa endelevu, na
imewataka wanafanyabiashara hao kuondoka mara moja, kinyume chake wataondaondolewa kwa nguvu.
Akizungumza
na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Msemaji wa Halmashuri
hiyo, Tabu Shaibu, alisema operesheni hiyo ni mkakati wa viongozi wa
halmashauri hiyo katika hali ya usafi.
Alisema
operesheni hiyo itaendeshwa katika kila eneo la wilaya hiyo, itawahusu
wale wote wanaofanyabiashara kinyume cha sheria za halmashauri hiyo
ambapo wale waliofuata utaratibu haitawagusa.
“Ujio
wa Obama unaweza ukawa sababu lakini lazima tukubali kuwa katika mila
zetu majumbani kwetu tumekuwa na ustarabu anapokuja mgeni huwa
tunajaribu kuyaweka mazingira yetu kwenye usafi”alisema Tabu. Tabu
alisema operesheni hiyo katika Mtaa wa Kivukoni iliaza jana kutokana na
ukweli kwamba huko ndiko kwenye Ikulu ya Rais na viongozi wengine wa
Serikali.
Kuhusu
polisi kushiriki kwenye operesheni hiyo, alisema uamuzi huo ulitokana
na viongozi wa Mkoa huo, hata hivyo lengo ni kushirikisha kila mdau wa
wilaya hiyo, hivyo si ajabu kuona polisi wanafanya hivyo.
Aidha,
wafanyabiashara hao walitakiwa kujaribu kujiunga kwenye vikundi na
kuomba maeneo ya kufanyia biashara kisheria kupitia viongozi wa Mitaa,
Kata hadi kwa Mkurugezi
0 comments:
Post a Comment