Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Wakati
mashabiki wengi wakidhani Mabingwa wa soka duniani, timu ya taifa ya
Kispania wangewafunga Tahiti mabao zaidi ya 10, hatimaye watoto wa
Tahiti wamekaza na kuwazuia vilivyo wapinzania wao na kufungwa maboa
10-0 tu.
Mshambuliaji
Fernando Torres amefunga mabao manne pamoja na kukosa penalti wakati
Hispania ikiifumua 10-0 Tahiti katika mchezo wa Kundi B Kombe la Mabara.
Alifunga
mabao hayo katika dakika za tano, 33, 57 na 78 wakati David Villa
alipiga Hat-trick katika dakika za 39,49 na 64, David Silva akafunga
mawili dakika za 31 na 89 na Juan Mata pia akafunga dakika ya 66
kuiwezesha Hispania kupaa kileleni mwa Kundi B mbele ya Nigeria, ambao
muda huu wanamenyana na Uruguay.
Kikosi
cha Hispania kilikuwa: Reina, Albiol, Azpilicueta, Ramos/Navas dk46,
Monreal, Martinez, Cazorla/Iniesta dk76, Silva, Villa, Torres na
Mata/Fabregas dk69.
Tahiti:
Roche, Ludivion, Vallar, Lemaire/Vero dk73, Aitamai, J Tehau, A Tehau/T
Tehau dk53, Vahirua, Caroine, Bourebare/L Tehau dk69 na Chong Hue.
Moto wa nguvu: Fernando Torres alikuwa hatari katika mchezo wa usiku wa kuamkia leo dhidi ya Tahiti
Hata mie: Mshambuliaji Barcelona David Villa naye alionesha kiwango cha juu
Kazi yaanza: Torres akitumbukiza goli la kwanza
CONFEDERATIONS CUP GROUP B
Team | Played | Won | Drawn | Lost | For | Against | Points |
---|---|---|---|---|---|---|---|
Spain | 2 | 2 | 0 | 0 | 12 | 1 | 6 |
Nigeria | 2 | 1 | 0 | 1 | 7 | 3 | 3 |
Uruguay | 2 | 1 | 0 | 1 | 3 | 3 | 3 |
Tahiti | 2 | 0 | 0 | 2 | 1 | 16 | 0 |
Lingine tena: Torres akiandika kimiani bao la pili
0 comments:
Post a Comment