Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akiandika kwenye daftari la
mwananfunzi aliyekaa pembeni yake kama ishara ya matumizi ya madawati
320 yaliyokabidhiwa na taasisi ya Hassan Maajar Trust ya jijini Dar
es Salaam tarehe 06-06-2013 katika shule ya msingi Kasense ikiwa ni
jitihada za taasisi hiyo kusaidia elimu nchini. Mkuu
huyo wa Mkoa aliishukuru taasisi hiyo na kusema mfano wake ni wa kuigwa
ukilinganisha na taasisi zingine ambazo huishia kuilamu Serikali na
huduma zilizopo badala ya kutoa mchango wowote. Kutoka kushoto ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Hassan Maajar Trust Bi Zena Tenga na Makamu
Mwenyekiti Ndugu Shariff Maajar. Wa tatu kutoka kushoto aliyesimama ni
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima.
Wanafunzi
wa shule ya msingi Kasense wakiwa wamekalia baadhi ya madawati
yaliyotolewa shuleni hapo na taasisi ya Maajar Trust. Jumla ya shule
nane (8) za Mkoa wa Rukwa kutoka kila Wilaya zenye upungufu mkubwa wa
madawati zimepata madawati arobaini (40) kila moja kuondoa upungufu
unaowakabili.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akizungumza katika hafla fupi
ya kukabidhi madawati 320 ya taasisi ya Hassan Maajr Trust kwa shule za
msingi Mkoani Rukwa tarehe 06-06-2013 katika shule ya msingi Kasense,
Mkuu huyo wa Mkoa aliishukuru taasisi hiyo na kusema mfano wake ni wa
kuigwa ukilinganisha na taasisi zingine ambazo huishia kuilaumu Serikali
badala ya kusaidia katika huduma za jamii. Aliendelea kusema kuwa
katika kuhakikisha huduma za elimu Mkoani Rukwa zinaboreka atakuwa
dikteta kuhakikisha kila mtu wakiwemo wazazi wanatimiza wajibu wao
katika kuhakikisha huduma za elimu Mkoani Rukwa zinaimarika. Kulia ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Hassan Maajar Trust Bi Zena Tenga.
Katibu
Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akitoa taarifa fupi ya
madawati kwa shule za msingi Mkoani Rukwa katika hafla fupi kukabidhi
madawati 320 ya taasisi ya Hassan Maajar Trust kwa shule hizo Mkoani
Rukwa tarehe 06-06-2013 katika shule ya msingi Kasense, Aliishukuru
taasisi hiyo na kusema kuwa Rukwa ina uhaba wa madawati 33,638 sawa na
asilimia 50.2%.
Makamu
Mwenyekiti wa taasisi ya Hassan Maajar Trust Bw. Shariff Maajar
akizungumza katika hafla fupi kukabidhi madawati 320 ya taasisi hiyo kwa
shule za msingi Mkoani Rukwa tarehe 06-06-2013 katika shule ya msingi
Kasense. Mwenyekiti huyo alisema kuwa lengo la taasisi hiyo ni kuboresha
mazingira ya kusomea watoto nchini Tanzania. Aliwaasa wadau wa elimu
Mkoani Rukwa kuchangia katika sekta hiyo kwa maendeleo ya taifa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hassan Maajar Trust Bi. Zena Tenga akisoma houtuba yake kwenye hafla hiyo.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akimkabidhi Makamu Mwenyekiti
wa taasisi ya Hassan Maajar Trust Bw. Shariff Maajar shilingi laki moja
na nusu ili aikabidhi kwa mwalimu mkuu shule ya msingi Kasense ikiwa ni
sehemu ya azimio alilolianzisha na kuliita “Azimio la Kasense” KADARU
(Kampeni ya Dawati Rukwa) katika hafla fupi kukabidhi madawati 320 ya
taasisi ya Hassan Maajar Trust kwa shule za msingi Mkoani Rukwa tarehe
06-06-2013.
Makamu
Mwenyekiti wa taasisi ya Hassan Maajar Trust Bw. Shariff Maajar
akizungumza katika hafla fupi kukabidhi madawati 320 ya taasisi hiyo kwa
shule za msingi Mkoani Rukwa tarehe 06-06-2013 katika shule ya msingi
Kasense, Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya,
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima, Meya Manispaa ya
Sumbawanga Sabas Katepa na Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya
Hassan Maajar Trust Bi. Zena Tenga.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akipima uelewa wa baadhi ya
wanafunzi wa shule ya msingi Kasense Mkoani Rukwa kwa kuwapa mtihani wa
kuandika wakati wa hafla fupi kukabidhi madawati 320 ya taasisi ya
Hassan Maajar Trust kwa shule za msingi Mkoani Rukwa tarehe 06-06-2013
katika shule hiyo, Kulia ni Mstahiki Meya Manispaa ya Sumbawanga Sabas
Katepa.
Kutoka
kushoto ni Makamu Mwenyekiti Hassan Maajar Trsut Bw. Shariff Maajar,
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya, Mstahiki Meya Manispaa
ya Sumbawanga Sabas Katepa na Mkurugenzi Mtendaji Hassan Maajar
Trust Bi. Zena Tenga wakifurahia Ngonjera ya wanafunzi wa shule ya
msingi Kasense katika hafla hiyo ya kukabidhi madawati.
Picha
ya pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya,
viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga na viongozi wa taasisi
ya Hasaan Maajar Trust.
(Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa – rukwareview.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment