Wednesday, June 19, 2013

SONY DSC 

Na Baraka Mpenja
Mtu mwenye pesa zake, keptein wa zamani wa jeshi la wananchi Tanzania JWTZ, Milionea  Zacharia Hans Poppe ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, mjumbe wa kamati ya utendaji na mratibu wa timu katika mashindano, leo jioni anatarajiwa kuhudhuria mazoezi ya Simba sanjari na wajumbe wa kamati yake.
Mnyama anaendelea kupiga jalamba la nguvu katika Uwanja wa Kinesi, Urafiki, jijini Dar es Salaam “Jiji la Majichumvi”. 
Poppe , aliyerejea Jumapili nchini kutoka Tunisia alipokwenda kufuatilia kitita cha mauzo ya mchezaji wao nyota Mganda Emmanuel Anold Okwi  katika klabu ya Etoile du Sahel ya huko yuko atafika uwanjani ili kuangaliwa wachezaji wao wakati huu ambapo wanaimarisha kikosi chao kurejesha ubingwa waliopokonywa msimu uliopita na watani wao wa jadi, Dar Young Africans.
Wachezaji wote Simba wenye makazi yao mitaa ya Msimbazi Kariokoo jijini Dar es salaam wapo  mazoezini  isipokuwa wale waliokuwa zao za taifa kwa maana ya Taifa stars ya Tanzania na Uganda katika mechi za kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia mwakani nchini Brazil.
Simba imepania kujiimarisha chini ya kocha mpya, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’ aliyekuwa na “Wanankulukumbi” Kagera Sugar msimu uliopita.
Aidha katika kuhakikisha wanafanya vizuri, Simba wanaonekana kuwa makini mno katika usajili na uundaji mzima wa kikosi cha msimu mpya.
Tayati imekwishasajili wapya kadhaa kuboresha timu, wakiwemo kipa Andrew Ntalla, Issa Rashid, Mganda Samuel Ssenkoom, Adeyoum Saleh Ahmed na bado natupia jicho la tatu maeneo mengine kusaka bunduki mpya.
Hivi karibuni walilamba dume, baada ya kumsainisha mkataba wa miaka miwili, kiungo mwenye kiwango cha juu zaidi kwa sasa ndani ya kikosi cha Stars na Simba, Amri Kiemba.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video