Omary
Tego yumo ndani ya kundi jipya la Raha ya Pwani Modern Taarabu chini ya
usimamizi wa mkurugenzi wa kampuni ya KFM, inayomiliki kituo cha redio
cha kifimbo fm kinachana anga kutoka kanda ya kati, Dodoma Tanzania,
Dkt. Kifimbo
Na Baraka Mpenja
Haya
haya wakazi wa Dodoma, baada ya kusikia burudani nyingi za miondoko ya
kipwani Pwani kutoka makundi mbalimbali, sasa wapenzi wa taarabu
wanajiandaa kupata burudani ya kukata na shoka kutoka kundi jipya la
“Raha ya Pwani Modern Taarabu” chini ya usimamizi wa kampuni ya KFM
inayojihusisha na masuala ya mawasiliano kwa umma.
Mkurugenzi
wa kampuni ya KFM inayomiliki kituo cha redio cha Kifimbo Fm
kinachorusha matangazo yake kutoka mjini Dodoma maarufu kama Kanda ya
kati, Dkt. Kifimbo ameimbia MATUKIO DUNIANI kuwa licha ya kampuni
yake kujihusisha na masuala ya mawasiliano kwa umma, imeamua kujikita
katika masuala ya burudani ili kuwapa mashabiki wake kitu roho inapenda
katika ulimwengu wa muziki wa taarabu.
“Unajua
watanzania wengi wanapenda masuala ya burudani, Kwa kutambua hilo,
kampuni yetu imeamua kuanzisha kundi jipya la muziki wa taarabu
lijulikanalo kwa jina la `Raha ya Pwani Modern Taarabu` ili kukonga
nyoyo za mashabiki wa redio yetu na watanzania wote kwa ujumla”. Alisema
Dkt. Kifimbo.
Dkt.
Kifimbo amesema uzinduzi rasmi wa kundi hili lililosheheni vipaji vya
kutosha utafanyika Julai 28 (mwezi wa saba) mwaka huu, katika ukumbi wa
burudani wa Kilimani Dodoma.
“Watu
wakae mkao wa kula, kundi hili litatoa burudani ya kutosha kwa
mashabiki wa taarabu. Kuna waimbaji wenye vipaji vikubwa wakiwemo
wakongwe na vijana. Yumo Mwanahawa, Shakira, Omary Tego, Issa Kamongo,
Abubakar Mzuri na Hassan Ally. Kuwepo kwa waimbaji hawa, Raha ya Pwani
Modern Taarabu lazima itese mjini”. Alisisitiza Dkt. Kifimbo.
Mkurugenzi
huyo wa KFM aliwataka mashabiki wa muziki wa taarabu kujitokeza kwa
wingi siku ya uzinduzi, kwani “Mwenye macho haambiwi tazama”, wasingoje
kusimuliwa.
0 comments:
Post a Comment