Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Safari
ya nyota wa soka duniani na klabu ya Real Madridi ya Hispania,
Cristiano Dos Santos Ronaldo sasa safari yake ya kurejea kwa mara
nyingine tena katika dimba la Old Traford imeiva baada ya kutolewa kwa
taarifa kuwa mshambuliaji huyo mwenye thamani kubwa zaidi duniani
anatarajia kukutana na maofisa wa Manchester United siku tatu zijazo ili
kujadili suala lake la uhamisho.
Nyota
huyo wa Real Madrid amekuwa akihusishwa kurudi nchini England baada ya
kutokea hali ya kutokuwa na furaha Bernabeu, lakini klabu hiyo ikajenga
imani kuwa Ronaldo angeendelea kukaa Hispania baada ya miamba hiyo
kumpata kocha mpya Carlo Ancelotti ambaye angemshawishi mkubaikia.
Gazeti
za Hispania la El Pais limeripoti kuwa nahodha huyo wa timu ya taifa ya
Ureno atakutana na maofisa wa United kabla ya kuanza mazoezi ya
kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu nchini Hispania na klabu yake ya
Reala Madarid.
Kanuni
za shirikisho la soka Duniani FIFA zinakataza timu kufanya mazungumzo
na mchezaji mwenye mkataba na klabu nyingine, lakini klabu hizo
zinashauriana kuzungumza, hivyo kumuongeza matumaini kocha mpya wa
United David Moyes kumsajili nyota huyo.
Lakini
kwa upande wa kocha Ancelotti alisema katika mazungumzo yake na
waandishi wa habari wakati wa kutambulishwa rasmi kuwa “Ronaldo ni
mchezaji mkubwa zaidi kuwahi kutokea, naona heshima kubwa akufanya naye
kazi”.
kocha huyo aliongeza kuwa aliwafundisha Zidane, Ronaldo De Lima, Ronaldinho, na anafurahi kumuongeza mreno huyu”.
Ancelotti
alipoulizwa kuhusu suala la kumnasa Radamel Falcao ambaye amesaini
Monaco, Anceloti alisema ni mchezaji mzuri sana, lakini ana wachezaji
wakubwa zaidi akiwemo Ronaldo, Higuain na Benzema.
Siku za hivi karibuni kocha mstaafu wa Manchester United Sir Alex Ferguson amekuwa akimhitaji Ronaldo kurejea Old Traford ili aisaidie zaidi timu yake iliyomptaia jina katika ulimwengu wa soka.
Wakati taarifa za Ronaldo kutimkia United zikizidi kushika kasi, tayari Rais wa Real Madrid alishasema kuwa nyota huyo mwenye thamani ya pauni milioni 80 kwa sasa atasaini mktaba mpya, lakini Ronaldo alikanusha suala hilo kupitia mtandao wa kijamii.
Siku za hivi karibuni kocha mstaafu wa Manchester United Sir Alex Ferguson amekuwa akimhitaji Ronaldo kurejea Old Traford ili aisaidie zaidi timu yake iliyomptaia jina katika ulimwengu wa soka.
Wakati taarifa za Ronaldo kutimkia United zikizidi kushika kasi, tayari Rais wa Real Madrid alishasema kuwa nyota huyo mwenye thamani ya pauni milioni 80 kwa sasa atasaini mktaba mpya, lakini Ronaldo alikanusha suala hilo kupitia mtandao wa kijamii.
Bado
anapenda sana: Ronaldo hakushangilia baada ya kufunga bao katika mchezo
wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya United na kuonesha kuwa bado
ana mapenzi makubwa na klabu hiyo
Ronaldo alikuwa nchini Indonesia na Rais President Susilo Bambang Yudhoyono kupanda miti
Bado anahitaji sana: Carlo Ancelotti anavutiwa kumfundisha Ronaldo
0 comments:
Post a Comment