Baada
ya kuzagaa kwa taarifa kuwa kiungo nyota wa klabu ya Simba na timu ya
taifa ya Tanzania, Amri Athman Kiemba “Jembe la kulimia katika kokoto”
kuwa alikuwa katika rada za Yanga ambao walitaka kuwaliza Simba kwa
kumsainisha mkataba, hatimaye ubishi waashi baada ya nyota huyo kusaini
mkataba na mnyama kwa kitita cha shilingi milioni 35.
Hatimaye
mazungumzo baina ya Klabu ya Simba na mchezaji Amri Kiemba yamemalizika
kwa pande hizo mbili kukubaliana kuongeza mkataba mpya, hivyo
kuwaondolea presha mashabiki wa Simba na Viongozi walikuwa na hofu ya
kupigwa bao na Yanga.
Mchana
wa leo Simba ilikuwa kwenye jitihada nzito kuhakikisha inamzuia Kiemba
kusaini Yanga kwa kumpa ofa nono ya mkataba mpya, Kiemba alikuwa
akihitaji kiasi cha millioni 38 ili asaini msimbazi lakini baada ya
mazungumzo marefu Kiemba amekubali kusaini kwa kiasi cha millioni 35 kwa
miaka miwili.
Pia
Kiemba atakuwa analipwa mshahara wa millioni 2 kwa mwezi. Alisaini
mkataba huo mbele ya kaimu makamu mwenyekiti Mzee Kinesi.
CHANZO CHA HABARI NI SHAFFIH DAUDA IN SPORTS
0 comments:
Post a Comment