Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
BAADA
kunusurika kufutwa, Mechi ya Timu za Taifa za Brazil na England
itachezwa leo Usiku huko Mjini Rio De Janeiro kwenye Uwanja wa Maracana,
ambao Jina lake rasmi ni Estadio Jornalista Mário Filho, ikiwa ni
ufunguzi rasmi wa Uwanja huo uliofanyiwa ukarabati mkubwa.
Juzi,
Jaji mmoja aliamua Mechi hiyo isichezwe baada ya Uwanja huo kutotimiza
masharti ya usalama lakini baadae uamuzi huo ukafutwa baada ya Rufaa.
Tangu
ufanyiwe ukarabati tayari Mechi moja ya maonyesho imeshachezwa
iliyowahusisha Mastaa wa zamani wakati Manguli wa Brazil, Ronaldo na
Bebeto, walipoongoza Timu tofauti hapo Aprili 27 na kushuhudiwa na
Watazamaji Elfu 25.
Maracana,
ambayo iliwahi kupakia Watazamaji hadi 200,000, ilijengwa kwa ajili ya
Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 1950 ambayo Wenyeji Brazil walifungwa
kwenye Fainali yake Bao 2-1 na Uruguay waliotwaa Ubingwa wa Dunia.
Kwa
mara nyingine tena, Maracana itachezwa Fainali ya Kombe la Dunia hapo
Mwaka 2014 wakati Brazil watakapokuwa Wenyeji na Uwanja huo utachukua
Washabiki 78,838 wote wakiwa wamekaa Vitini.
Wakati
huo huo beki wa Brazil na klabu ya Chelsea ya London, David Luiz
amesema England hawana uwezo wa kutwaa kombe la dunia mwakani
litakalofanyika nchini humo.
“England hawawezi kushinda kombe la dunia. Hawana mawazo hayo kwa sasa na itakuwa ngumu sana kwao”. alisema Luiz.
Luiz aliongeza kuwa “Niliwatazama kombe lililopita, hawakucheza vizuri, na mpaka sasa hawajabadilika hata kidogo”.
Nyota huyo ataitumikia timu ya taifa katika mchezo wa leo wa kirafiki dhidu ya England.
Mpiganaji:
David Luiz akiwania mpira na nyota mwenzake Luis Felipe wakiwa
mazoezini kujiandaa dhidi ya mchezo wa leo dhidi ya England
Luiz amekataa kabisa kuwa England inaweza kutwaa taji la kombe la dunia
Maskini: England walibanwa mbavu baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Republic of Ireland
0 comments:
Post a Comment